UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
Academic Staff Assembly
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 2/3/2013


Utangulizi

Wapendwa waandishi wa habari. Tunaomba kupitia ninyi tuweze kuongea na watanzania wenzetu kuhusu hali ya amani ilivyo nchini mwetu kufuatia kila aina ya dalili ya watanzania kukosa uvumilivu wa kidini. Tunatambua kuwa serikali yetu imefanya mambo mazuri mengi tu nchini, hilo hatuna mashaka nalo; hata hivyo kama watanzania tunadhani kuna baadhi ya mambo hayaendi sawa. Hivyo basi, tunaomba kuchukua nafasi hii kuelezea wasiwasi wetu kuhusu migogoro hii ya kidini inayozidi kukua nchini.

Migogoro hii ilianza kuvuka kama moshi lakini sasa inaanza kulipuka na kusambaa zaidi. Tumeshuhudia uchomaji moto wa kanisa kule Mbagala, kumwagiwa tindikali shekhe mmoja kule Zanzibar na Shekhe mwingine kuuawawa, kuchomwa makanisa Zanzibar, kupigwa risasi viongozi wa kikristo kule Zanzibar na pia mgogoro wa kuchinja huko Geita ambako tumeshuhudia mchungaji mmoja akiuawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Nimesoma tamko lote. point ninayoona ya maana ni ile
    inayozungumzia usawa wa elimu. Angalau haijaegemea upande wa dini yoyote.

    Napenda kuongezea katika matamko ya mwisho yasimayo : "Pia, ni muhimu sasa,
    kila dini iendeshe maswala yake bila kutaka kubebwa na serikali"
    Nyongeza yangu ni kwamba kama kuna mikataba au makubaliano yoyote
    kati ya serikali na dini fulani yavunjwe mara moja.

    Baba wa taifa alikuwa mdini tu. Mimi nadhani tunapopiga vita dhidi ya
    migogoro ya kidini nchini Nyerere asitumike kama reference, otherwise baadhi
    ya watu hapa nchini wikiona maelezo yenye kiambatanisho cha Nyerere wanakuona
    wewe ni mdini tu.

    Haya ni maoni yangu kulingana na hali ya kidini ninayoiona hapa nyumbani.

    ReplyDelete
  2. Mimi nahisi kwa ukweli ni lazima tuukubali na tuache kutizama mambo kisiasa au kwa malengo ya chama fulani ,Serikali inafaa kulaumiwa kwa hili kwa mfano waziri Mkuu alisema kwamba linapotokea hitilafu yeyote ile ni vizuri watu kukaa pamoja na kujaribu kuzungumza ili jambo lolote liweze kupatiwa ufumbuzi,na hivi ndivyo ilivyo kwa jamii yeyote ile Duniani,lakini watu wamechoka na ndipo wanaamuwa kuchukuwa sheria mikononi mwao na hii ni mbaya sana kwa jamii, ninasema hivyo kwa mfano unapokwenda POLISI kuripoti ua kusitaki kitu Polisi wanakuwa hawafanyi kazi yao kwa uwadilifu ,zarau ndio zaidi,hawafuatilii lolote na ndipo watu inafikia kuchukuwa uwamuzi mikonini mwao, serikali ni lazima hili jambo waliangalie kwa umakini na jeshi la polisi ni lazima wafanye kazi kwa uadilifu ili kuepusha matatizo kati ya wananchi wenyewe.Kwa upande wa ZANZIBAR mimi nahisi sifikirii kama wazanzibari wana chuki au tatizo la aina yeyote na watu wenye imani tofauti au wenye kuamini Dini tofauti isipokuwa Wazanzibari wanachotaka nimaadili yao hulka zao kalcha yao kuheshimiwa na kuzingatiwa na sio watu wanakuja kwenye nchi yao na kuanza kuvuruga utaratibu wao na kalcha zao ambazo wamerithi tangu babu na mababu zao na sio Wazanzibari tuu popote duniani unapoanza kuvuruga utaratibu wa kalcha na madhehebu wa watu wenyewe hawatokubali katu ,Leo Zanzibar watu wanakuja na kuanza kufunguwa madanguro ya kujiuza,pombe za kienyeji,nguo wanazovaa hazieleweki na mengineyo ,hilo popote pale halikubaliki,ni lazima tukubali unapokwenda kwenye nchi ya watu ni muhimu kuheshimu mila na desturi zao vyenginevyo utasababiha matatizo,na Hilo ndio tatizo la Wazanzibari,Ni lazima kuheshimu mila na desturi za watu hata wazungu kila nchi ulaya ina desturi zake na utamaduni wake na kamwe hawakubali mtu yeyote kuwaingilia kwenye hilo.

    ReplyDelete
  3. Wewe hapo juu unaongea usilojua pengine kutokana na propaganda uliyolishwa kuwa wewe au wenzako walionewa, Kwani uelewa wako unahusishwa vipi na rais wa nchi. Ina maana huyo rais unayemsema bado yupo madarakani? Mbona ni miaka nenda imeshapita na kuna baadhi ya mikoa inafanya vibaya. Kukusaidia tu unatakiwa usome kwa bidii na uondoe mawazo potofu kuwa wewe au kikundi fulani mnahitaji msaada fulani vinginevyo utaendelea kujazwa propaganda na watu wasio na elimu ya kutosha na kuanza kujifunga mabomu. POLE SANA.

    ReplyDelete
  4. Kwanza Kabisa mie napenda kutoa mchango wangu wa mawazo siko mbali na mtoa Mada ..mie nasema hivi ile mihadhara inayoendeshwa kwenye sehemu za wazi kubishana kati ya wakristo na waislamu yafutwe kabisa ,na kama kuna dini itaizungumizia dini nyingine kwa mabaya mhusika atakayekuwa katamka akamatwe na kufungwa miaka isiyopungua 30.nadhani hapo ndio tutamaliza tatizo hili,lkn hapa serikalini ,ndio wanaoeneza udini wanakemea vitendo hivyo kwa maneno tu na sio kwa vitendo ,kwa sababu ndio wanawatuma hao wanaokashfu dini zingine!!tumeseme tu ukweli.Naomba rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania apige marufuku kabisa mihadhara ya kubishana kati ya Dini moja na nyingine.

    ReplyDelete
  5. Masikitiko yangu ni kuwa tuna wasomi wanasema nadharia zinazozungumzwa mitaani bila data.

    Na tatizo hata mapendekezo yako hayatekelezeki kiserikali kwani yataleta matatizo zaidi. Kuishauri serikali kunyima vyombo vya habari uhuru hakudumishi amani. Kumbuka uhuru ni kuweza kusema lolote hata kama linamuudhi mtu almuradi si tusi. Na kila mtu ajuwe kila amtu ana uhuru wa kusema mawazo yake hata kama ni mabaya.

    Angalia mi msomi suluhisho langu sasa:

    Pamekuwepo na manung'unukio ya udini kwa miaka mingi. Data zimekuwa ni idadi ya waajiriwa serikalini inaonyesha dini fulani imejaa. Pia elimu ya juu (wahadhiri na wanafunzi) wengi ni dini fulani.

    Kimsingi malalamiko ni ya msingi lakini kiini cha tatizo kimekuwa kikipuuziwa. Matatizo yanasababishwa na vyanzo vya ndani (ya waumini) na vyanzo vya nje.

    Tatizo walalamikaji hawakubali vyanzo vya ndani vya tatizo na hueleza vyanzo vya nje tuu (yaani udini). Tatizo sambamba pia ni watatuaji wa tatizo hawakubali kutatua matatizo ya vyanzo vya nje wanataka vyanzo vya ndani tuu (kama vile ubaguzi haupo na hawapendi shule). Mtazamo wangu ni kwamba vyanzo vyote vya tatizo ni halisia.

    Zao la tatizo limekuwa kukomaa kwa tatizo kwani halitatuliwi. Hakuna kiongozi mkubwa anayetaka kulitatua kitaalamu na wala hakuna mwongozo wa kikatiba wa kutatua udini. Bila mwongozo bali utatuzi utakuwa na tatizo zaidi. Mfano, utatuzi wa udini si kupata raisi wa dini fulani kutumia madaraka yake vibaya kuwapendelea wanaodhani kuonewa. Hilo litafanya raisi wa dini nyengine kuonea pia na nchi itakuwa jalala. ufumbuzi unatakiwa uwe kikatiba na kisheria kivitendo.

    Kama udini upo basi usipewe majibu rahisi. Sitarajii kama kuna kiongozi mdini atakubali upo. Na pia tafsiri ya neno udini iko chali, wengi wamaanisha kusali saana badala na siyo kumbagua mtu kwa misingi ya dini.

    Serikali, badala ya tuu kulaani ubaguzi, inatakiwa ianzishe sheria ya kuwaadhibu wadini katika sekta za serikali. Laana ni maneno matupu hayavunji mfupa. Laana hizi zinafanya udini uendelee kukuwa zaidi ya sasa. Na unaweza kukuta hamna hata mmoja katoa wazo hili kwa katiba mpya. Nani atoe? Tumezoea mtu akisema kuna udini nasi twamzomea yeye mdini. Nani anataka kuzomewa? Hapa hakuna kiungo cha kutolea maoni huru.

    Tumejitolea hadi damu kukomesha ukaburu nje lakini tumeshindwa hata kukubali kuwepo ukaburu ndani ya nchi. Kwa nini, tunadhani kukubali upo ndo kuukuza badala ya kuwa ni hatua ya mwanzo kuuondoa. Mficha ugonjwa mauti yalimuumbua.

    Brain wash? Kila mtu mwenye wazo tofauti na lako kawa brainwashed!

    ReplyDelete
  6. The report reveals something unexpected; the writer has little analytical skills. If majority of lecturers approve of this report I am not surprised we have 60% div V.

    The report lacks balance and concentrates on effect as opposed to real causes. Most causes are a bunch of simple answers lacking careful thought to a killer problem.

    In-depth research is needed to address the problem. Researchers perfect for the topic should not come from any religious group or expect bias. Bias will be due to their avoiding saying negative things about their religion. Who wanna go to hell?

    Sawa na kamati ya matokeo ya mtihani, walalamikaji ndo wanakamati unategemea nini? Bias!

    Kisingizio: eti kushirikisha wadau woote. Hapa hatupigi kura tunatafuta suluhu ya kitaalamu.

    ReplyDelete
  7. Mtoa mada umechokoza ila kuweka kwenye blog hii ya sisi ambayo hata sie akina kajamba nani tunatumia, basi tutakujibu.

    Kabla ya waarabu kuingia (wakiwa wageni wa kwanza) wenyeji yaani tuseme sisi tuliokuwa kwenye bara hili tulikuwa na dini zetu. Tuliishi kwa amani zaidi zaidi vita kila kukicha sababu ya kugombania milki ya ardhi na mifugo. mbali mbali zilikuwa na imani zao. Koo ziliogopa mizimu na miungu ya koo nyingine hivyo watu waliogopa kudhuriana ili wasije wakajikuta matatani.

    Uislamu ullitangulia ndipo na ukristu ukaja. Nadhani vile vivutio kwenye dini viliwafanya watu wachague wapi pa kwenda ingawa bahati mbaya kwa watumwa, wenyewe ilibidi wafuate dini za mabwana wao na do maana watumwa wengi hata baada ya kuokolewa lakini walijikuta wakiwa na dini hizo za kiislamu.

    Upande wa wakristu wengi walipenda kwenda shule, hivyo ilibidi wabatizwe ili waweze kusoma na ukawa mwanzo wa yote hayo. Baadaye dini zikawa za kurithikwenye familia ingawa tumeona kuna familia zenye mchanganyiko wa watu watu wenye imani tofauti.
    Mimi wakati nasoma kwenye miaka ya sitini na tatu mpaka namaliza primary tulikuwa na vipindi vya dini zote mbili na kila dhehebu lilikuwa na walimu. Watoto wa kiislamu walikuwa na chumba cha kuswalia kila siku wakati tupo boarding school. Shule yangu ilikuwa inaendeshwa na masista lakini waislam walikuwa wakipikiwa ftari nadaku wakati wa ramadhan. Kila Ijumaa hatukuwa na vipindi vya masomo kuanzia saa saba sababu waislam walikwenda msikitini na hivyo tulifanya masomo kama kujitegemea au liblary.


    Secondari niliyosoma mambo yalikuwa hivyo, Ingawa ile shule ilijengwa na serikali ya mwingereza lakini iliheshimu dini zote. Tuliabudu wote sikuona shida yoyote.

    Tatizo nimekuja kuliona siyo zamani nadhani kwenye miaka ya tisini waliporazimishwa watoto wa kike wa kiislam kufunika vichwa. Hapo tulianza kuona jinsi nchi iliingia kwenye tatizo la wao na sisi!!! Kwanini mtoto wa shule alazimishwe kuutangazia umma kuwa yeye anatoka familia ya kiislam na kwanini awe msichana tu na siyo vulana pia???
    Je dini mpaka utambulishe dunia au ipo rohoni mwako?

    Mchangiaaji toka Zanzibar sikubaliani naye anaposema kuwa waZanzibari wanachukia watu wanaoharibu mila zao. Dunia ni kijiji sasa hivi hakuna sehemu yoyote duniani uatakapokuta watu wanalazimisha watu wengine kufuata mila zao. Wazanzibari wengi wapo London lakini utakuta wamevaa hijab, je hilo ni vazi la waingereza? Nenda Sweden uone waswede wanavyochukia watu wanaovaa vile lakini bado wanawavumilia je wakisema basi kama unataka kukaa kwetu na wewe va kimini, utavaa au utafanyaje?

    Kijijini kwetu huwa tuna utaratibu wa kununa ng'ombe wakati wa Pasaka na Noel na kuchinja halafu tunagawana nyama, Je haturuhusiwi kujichinjia? na je hiyo ni sheria ya nchi?

    Tumefika pabaya sana sasa hivi kiasi mpaka unajiuliza, hao watu ninaowaona sasa wanavaa vitambaa, mbona tulikuwa wote mashuleni, makazini na hawakuwahi kujitambulisha na mavazi hayo iweje miaka hii saba wabadilike ghafla na kuvaa hijab kulikoni je kuna mkono wa mtu?

    Vyombo vya habari ni sauti ya watu vikizibwa midomo ndo tunakaribisha redio ugali ambapo kila anayeshiba ugali anatangaza yake mitaani na mitandaoni.

    Wasomi shaurini viongozi wetu waache kuingiza siasa kwenye kila kitu. Lini Askofu anayemiliki kanisa akateuliwa kuwa ubunge tena viti maalum? mbona Askofu wa kikatoliki hajawahi kuwa waziri hata kuwa kwenye tume kama walivyoteuliwa mashekh kwenye tume ya Pinda.

    ReplyDelete
  8. Anon wa Sun Mar 03, 01:41:00 pm 2013,
    Mtoa mada ansema wewe ndo tatizo, kuwashwa na dini isiyo yako. Inaonyesha unashindwa kuvumilia watu wawe tofauti na wewe. Fumbo umefumbiwa.

    Mbona unasema umesoma lakini unashindwa kutambua uhuru wa ibada? Kama dini yao inasema wasichana wajifunike we inakuuma nini? kwani watoto wako? au wamekulazimisha uwafunike wako? Au kutahiri wavulana we inakuwashiani.

    Pia unashindwa kuona kuwa dini ziko tofauti, yako ni ya rohoni ya wenzako ni roho na mwili. Kwa nini hutaki kuvumilia tofauti?

    Hiyo miaka 7, kama wameamua kufuata mstari ambao walikuwa hawafati kabla we inakwashiani?

    Mbona wewe mwaka huu unataka kuchinja imekuwaje mbona ulikuwa huchinji kabla?


    Kimsingi watu kama wewe ndo tatizo la taifa, na kusema umesoma kisomo hakikusaidii na ni ishara elimu ya bongo uchovu tuu.



    ReplyDelete
  9. Kwanza hapo UDSM ndo pamejaa UDINI, tangu chuo hicho kianzishwe hakijawahi kutoka VC muislam, pamoja na professor wote waislam waliopo nchi hii. Pia 99 % ya wakuu wa idara ni WAKRISTO, pamoja nauwepo wa wahadhiri waandamizi waislam wenye sifa za kuwa wakuu wa idara!

    Lakini pia hata ajira zipo kiupendeleo zaidi, kama ni muislam utafanyiwa mazonge wee mpaka nafasi ya ajira utaikosa! Wajitazame hao UDASA wenyewe, waislam ni wangapi?

    Hili tamko lao halina tofauti na tamko la MAASKOFU!

    Wabeja sana!

    ReplyDelete
  10. Anon wa Sun Mar 03, 01:41:00 pm 2013,

    Wewe ni wale watanzania ambao dini ya mwenzio ni tatizo lako. Wewe ni mlengwa wa mada ila hujijui. Yaani bila kuelewa mada umekimbilia kutoa komenti na kujianika.

    Wewe ukiwa mwajiri sijui kama unweza kumwajiri wa dini nyengine hata kama sifa anazo na atazalisha faida kazini.

    Tatizo wapo wengi kama wewe serikalini na kwenye vyuo vya uma, hao ndo wanakuza ubaguzi.

    ReplyDelete
  11. Here we go again.

    The highest learning institution in the country fails to look for informed sustainable solutions and headlongly goes for myths. It is easy to see that the ideas in this piece are not original.

    Description of the problems and solutions have been around on streets for ages. They are argued by commons and the solutions don’t match the problem as they have never worked.

    To my surprise, the so called professors have summarized the legends and fixed their academic seal to legitimize and make the legends genuine. A true sustainable solution does not need backing with a seal. It doesn't become true by the seal. It is unethical to stamp solutions that will only hurt the country, like the government having to go after press.

    The analysis in the piece lacks intellectual element and is incomplete as it ignores factors that would probably hurt writers' feelings.

    No surprise UDSM always tails behind SA and Egyptian universities but keeps going lower in ranks.

    Heko wataalam wa ndani, wasomi ndo ninyi ndo maana nchi haiendelei.


    ReplyDelete
  12. The report is not authentic as is not signed by any official of the assembly.

    I have reasons to believe this is not a work by the UDSM.

    Solutions listed are not learned and are likely to aggravate the problem. It is unlikely this is professors' work.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...