Mpishi Mkuu wa Bar ya Victoria Princes, Joseph Swai akishangilia mara baada ya kutangazwa mshindi wa fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma Mkoa wa Mwanza yaliyofanyika katika viwanja vya furahisha mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, Amina Masenza (kulia) akimkabidhi kitita cha shilingi milioni moja Joseph Swai wa Bar ya Victoria Princes mara baada ya kuibuka mabingwa wa fainali za mashindano ya Safariri Nyama Choma yaliyofanuika katika Viwanja vya furahisha mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Mpishi Mkuu wa Victora Princes, Joseph Swai akishangilia na kitita cha shilingi milioni moja mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Amina Masenza (kushoto kwake) ikiwa ni Mabingwa wa fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma 2013 Mkoa wa Mwanza yaliyofanyika katika viwanja vya furahisha mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja mauzo na usambazaji wa kanda ya ziwa , Malaki Sitaki na Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Mchina ambaye hakutambulika jina lake akicheza wakati Bendi ya Africana inatumbuiza wakati wa fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma yaliyofanyika katika Viwanja vya Furahisha mwishoni mwa wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Wachagga kwa nyama choma bwana. Mpaka Mwanza wamo!!!!

    ReplyDelete
  2. Lini kutakuwa na mashindano ya mboga za majani na masalad etc - nyama in hatari zake!!

    ReplyDelete
  3. bwana joseph swai naona hata kushangilia anashangilia kwa style ya kabila lao(M4C)
    hawa jamaa ni noma...!

    ReplyDelete
  4. BONGO haswa raha..ona mchina anavyofurahia-lol

    ReplyDelete
  5. Mwekezaji akikata mauno chezea mchina weye?

    ReplyDelete
  6. HAHAHA! Eti mwekezaji ananengua!

    ReplyDelete
  7. nyama choma inadhaminiwa na ulevi maana ndio vinaendana sasa wadau hapo juu msishangae shindano hilo kufanyika

    na kwa ushamba uliotukuka watanzania bado tunashangaa watu wenye asili ya asia au ulaya wakifanya jambo lolote hata kama ni jambo la kawaida kwa jamii

    ReplyDelete
  8. hivyo vidole Swai, wakati unashangilia, ni alama ya nini au una maana gani meku?
    Brain

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...