Meneja Idara ya wateja wakubwa wa Vodacom Tanzania Bi.Stela Mamuya akigawa msaada wa pedi za kisasa zinazofuliwa na zenye uwezo wa kudumu kwa mwaka mmoja pamoja na nguo za ndani kwa wanafunzi wakike wa shule za msingi Barazani na Qambasirong zilizoko Haydom wilayani Mbulu mkoani Manyara,msaada huo uliotolewa na Vodacom Foundation umegharimu zaidi ya shilingi Milioni saba.
Mfanyakazi wa Idara ya wateja wakubwa wa Vodacom Tanzania,Bw.Simon Martin akimkabidhi pedi za kisasa zinazofuliwa na zenye uwezo wa kudumu kwa mwaka mmoja pamoja na nguo za ndani mwanafunzi wa kidato cha sita Bi.Getrude Boniphace, zilizotolewa na Vodacom Foundation kama msaada kwa wanafunzi wa shule za msingi Barazani na Qambasirong zilizoko mkoani manyara,thamani ya vifaa hivyo vimegharimu zaidi ya shilingi milioni saba,anaeshuhudia katikati ni Mkuu wa kitengo cha msaada kwa wateja wakubwa Bw.Ally Zuber.
Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon,akimfundisha mtoto wa kidato cha saba Sarah Moses,namna ya kutumia pedi ya kisasa zinazofuliwa mbele ya wanafunzi wenzake,Vodacom Foundation ilitoa msaada wa pedi za kisasa zinazofuliwa na kudumu kwa muda wa mwaka mmoja pamoja na nguo za ndani, kwa wanafunzi wa shule za msingi Barazani na Qambasirong zilizoko Haydom wilayani Mbulu mkoani Manyara,uliogharimu zaidi ya shilingi milioni saba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. INAMANA NYIE VODA MUMEAMUA KUTOA MLICHOTAKA TU KUTOA MLIVYO WAULIZA WANAFAUNZI HAO HIVYO NDIVYO WALIVYOTAKA JAMANI NYIE,HIVI MNAVYOSHAURIANA HAMWEZI KUJUA MAWAZO YA KUFANYIA KAZI NA MENGINE YA KUACHA .HUO MSAADA ,MLIOTOA SIO WA KUJITANGANZA JAMANI AIBU SANA HIYO .TOENI VITABU ,TOENI HELA ZA KUWALIPA WALIMU BINAFSI KWA SHULE AMBAZO HAZINA WALIMU.fanyeni vitu vya msingi.
    .michuzi hii komenti naomba uiweke bana.

    ReplyDelete
  2. THIS IS AN INVENTION FOR SURE! VODACOM NEEDS TO FILE A PATENT FOR THIS!

    ReplyDelete
  3. Wewe uonagi wakijenga mashule ,kutoa vitabu na misaada ya kiafya .

    ReplyDelete
  4. na wajega huku kwetu Busekera karibu na Mlima Mtiro, Mara Ragion.

    ReplyDelete
  5. Picha ya chini jamani ktk Elimu Tanzania kuna KIDATO CHA SABA?

    AU NDIO MTIKISIKO WA MATOKE MABOVU YA KIDATO CHA 4 NDIO IMEBIDI TUPANDISHE WATOTO VIDATO HADI KIDATO CHA 7 ???

    ReplyDelete
  6. Mkishagawa hizo pedi nani atawafundisha jinsi ya kuzitumia?Halafu kibaya zaidi anaegawa ni dume zima ilhali akina dada wanatazama pembeni!!!!

    ReplyDelete
  7. huko kuna shida ya maji halafu mnapeleka pedi za kufua kutasomeka?????

    ReplyDelete
  8. Unapeleka madawati, vitabu na kujenga madarasa na bado unagundua watoto hawaendi shule. Hapa lazima tafiti ilionyesha kuna kitu. kinachotakiwa ni watoto kuwa shule wakati wote.

    Kufua kwani nguo wanazo vaa hazifuliwi? si naona hapo wako safi kabisa though safi ya kijijini.

    watu wengine bana!! unaona kabisa comments from non creative minds. unaandika tu.Dah watanzania zetu kelele tu!

    Vodacom BIG UP for this creativity!

    Mdau ughaibuni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...