Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen akiwaonesha waandishi wa habari timu wanazocheza wachezaji wa Morocco katika vilabu vya Ulaya. 
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen akifafanua jambo wakati akitangaza kikosi cha wachezaji 23 watakaoingia kambini kwa ajili ya mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakaofanyika mwakani nchini Brazil.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 23 watakaoingia kambini Jumamosi (Machi 16 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi ya mashindano dhidi ya Morocco.
Mechi hiyo ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma, Machi 17 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Nassoro Masoud Cholo (Simba) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
SEMINA ELEKEZI COPA COCA-COLA KUFANYIKA MACHI 19
Semina elekezi kwa ajili ya michuano ya Copa Coca-Cola 2013 itafanyika Machi 19 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Washiriki wa semina hiyo wanatakiwa kuripoti Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) siku moja kabla (Machi 18 mwaka huu).
Washiriki hao ni makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar. Pia waratibu wa mikoa wa mashindano ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).
Barua za mwaliko kwa ajili ya semina hiyo tayari zimetumwa kwa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa.
Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF
                                      

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kuna kijana yuko Bwawa la Maini-Liverpool(Ankal upo?) inaitwa Oussama Assaidi.Huyu Kijana ni hatari sana na anatakiwa kupewa Ulinzi mkali kama atakuja.Anacheza Winga ya kushoto.Liverpool hawamtumii sana kwenye Ligi kuu ya Uingereza,anacheza mechi za Europa League na alikuwa Afrika ya kusini kwenye michuano ya AFCON2013.Ana kasi,anamiliki mipira,na anapiga chenga ni balaa

    David V

    ReplyDelete
  2. Sasa TFF na serikali muweke tofauti zenu pembeni na muungane na Kilimanjaro Premium Lager kuhamasisha wananchi tujitokeze kwa wingi kuchangamkia na kuipa support Taifa Stars. Hatutakuwa na chance nyingine kama hii ya kuonyesha maajabu - just imagine tukishinda mechi hii tutakuwa katika nafasi nzuri kwelikweli kuweka historia kwenda WC2014 from East Africa!

    ReplyDelete
  3. kwenda world cup kutabakia kuwa ndoto hivi kweli hata kama mchezo ni kujiamini lakini jeuri ya kumfunga morroco hatuna

    ReplyDelete
  4. jamani naomba nijuzwe kidogo kuna jambo sijalifahamu

    hivi wachezaji wa mazembe ya drc congo wanahesabika kama wachezaji wa tanzania taifa stars?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...