Salaam, Ankal 

naomba upokee picha za uchaguzi Mkuu wa Kenya unaondelea leo katika maeneo mbali mbali.Hapa ni kutoka kituo kimoja tu cha Moi Avenue. Watu ni wengi mno, wengine wamekuwa kwenye foleni tangu saa kumi alfajiri. Uwezekano wa wote kupiga kura kabla ya saa kumi na moja sidhani kama utawezekana.

Mdau 
Hassan Mhelela

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kazi ipo Kenya,
    Liende liende,
    Bora salama!

    ReplyDelete
  2. La muhimu safari hii Wakenya kwa mara ya pili tena msichinjane!

    Licha ya gharama kubwa sana za Uchaguzi wa Kitekinolojia nimeshangaa kusikia pana Vituo vingine wamelazimika kupiga Kura kienyeji baada ya vifaa kuchelewa kufikishwa Vituoni asubuhi!

    Hii kweli ndio bei halisi ya Demokrasia hapa Afrika?

    ReplyDelete
  3. Gharama chafu za Uchaguzi na Tekonolojia iliyotumika havilingani na tukio kama hili la kushindwa kupiga Kura wote leo!!!:

    Uchaguzi umegharimu Fedha chafu saana sioni kwa nini wote wasipige Kura!

    Kwa Tekinolojia yote hiyo kwa nini hadi sasa saa 11 imeshapita wasiwe wamekwisha Piga Kura?

    ReplyDelete
  4. Kwa Technology ya Kisasa iliyotumika nilitegemea watamaliza kupiga Kura masaa matatu (3) kabla ya muda !!!

    ReplyDelete
  5. Hizo sehemu walizopiga Kura holela bila Technology kwa kuchelewa kufika vifaa, wasije kuanza kuhesabu Kura kwa mikono yakatokea ya Uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2004 Muhula wa Pili wa Raisi G.W.Bush!!!

    ReplyDelete
  6. Kwa kweli hadi sasa Mchakato wa kuhesabu Kura za Uchaguzi unaendela shwari, tunamhsukuru Mungu kwa kuwaongoza Wakenya wakawa na busara hizi.

    Lakini nadhani hata atakayeshindwa atakubaliana na Matokeo.

    Kama pia Wapinzani nchini Tanzania watakuwa na busara hizo, tofauti na tulivyo shuhudia MGOMBEA WA CHAMA CHA UPINZANI TANZANIA (Chama kapuni) ALIVYOKATAA KUMTAMBUA RAISI MTEULE UCHAGUZI WA MWAKA 2010 HADI ANAALIKWA IKULU LAKINI CHA AJABU ALIPOKEA MWALIKO NA AKAAMBATANA NA WENZAKE!

    ,,,,Naahidi kama Mgombea Uraisi Tanzania wa Upinzani atakubali,,,Mimi Sele Chinga Mkazi wa Mtwara Mwana CCM na Yanga Damu naaahidi ''KUJAMBA KI-DIGITALI'' humu online kwa Michuzi,,,!

    ReplyDelete
  7. Leteni za Maendeleo ya Matokeo sasa Kenya!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...