Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe,akisisitiza jambo kwa Waziri wa Uingereza anaeshughulika na Maswala ya Afrika, Bw. Mark Simmonds(kushoto kwa Waziri Mwakyembe), wakati Waziri huyo alipomtembela ofisini kwake mwishoni mwa wiki kujadiliana maswala mbalimbali yanayohusu Usafiri wa Anga, Reli pamoja na bandari.
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe(mwenye suti nyeusi) akimuonyesha Waziri wa Uingereza anaeshughulika na Maswala ya Afrika, Bw. Mark Simmonds Miradi mbali mbali inayofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kwa hapa Tanzania. Waziri Mwakyembe alikutana na Waziri huyo ofisni kwake kujadiliana kuhusu Usafiri wa Anga, Miradi ya Bandari na Miradi mbalimbali ya Reli mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Serikali ya Uingereza anaeshughulika na Maswala ya Afrika, Bw. Mark Simmonds akifafanua jambo kwa Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwkyembe(Mwenye suti Nyeusi), wakati alipomtembelea waziri Mwakyembe ofisini kwake mwishoni mwa wiki. Kulia kwa Waziri Mwakyembe ni Balozi wa Uingereza Tanzania, Dianna Melsone.
Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harrison Mwakyembe akishikana mikono na Waziri wa Uingereza anaeshughulika na Maswala ya Afrika, Bw. Mark Simmonds, wakati alipomtembela ofisini kwake leo huu.
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Uingereza anaeshughulika na Maswala ya Afrika, Bw. Mark Simmonds(mwenye tai ya blue bahari), Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melsone(kushoto kwa Waziri Mwakyembe) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo(Kulia kwa Waziri Mark).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Oohh angemuomba aongee na British Airways wasikache route ya Dar-London

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...