Kamanda wa vyuo vikuu nchini Moses Katabalo (pichani) akitoa maoni yake kwa waandishi wa habari ( hawapo pichani ) ofisini kwake jijini Dar es Salam jana kuhusu hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa , hivyo amewataka wanafunzi kutojiingiza kwenye migogoro ya masuala ya udini na kiushi vizuri kwani wanategemeana katika masomo na maisha, iwapo watafarakana athari zake ni kubwa.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Taifa na Mwenyekiti wa tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM )Seki Kasuga pichani akitoa maoni yake kuhusu hotuba ya mwisho wa mwezi aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni, Seki amewashauri wanavyuo nchini kutobaguana, kushikamana ili kuendelea vizuri kwenye masomo yao pamoja na kujiepusha vitendo vitakavyoleta migogoro.
Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam anaechukua masomo ya sayansi Halima Ahmad (pichani) akichangia hotuba ya mwisho wa mwezi aliyoitoa Rais Kikwete kuhusu amani na utulivu nchini , amesema wanavyuo wasikubali kutumiwa katika kuleta migogoro isiyokuwa na manuafaa kwa taifa letu, bali waendelee kutafuta elimu kwa faida yao pamoja na maendeleo nchini.Picha na Mwanakombo Jumaa- (MAELEZO).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. UDINI:

    Mara zote ukishaona mahala pana Ajenda za Udini, tazama kwa makini nyuma yake panakuwa na Siasa.

    1.Mfano unaweza kusoma Gazeti lenye Kichwa cha Habari kinachogonga akili, lakini utakapo lichukua ukasoma habari inakuwa ni tofauti na Kichwa cha habari ukurasa wa mbele!

    2.Ukosefu wa kazi au mipango ya kufanya huchangia kuwashawishi watu kuelemea sana ktk harakati na Siasa zisizo na tija.

    Hivyo mara zote vurugu na matatizo ynayowasilishwa kupitia harakati za Kidini kunakuwa na maslahi ya Kisiasa, hivyo tuwe makini sana na nyendo zetu na jinsi tunavyo yapokea mambo yanayoelekezwa kwetu.

    Kwa bahati mbaya zaidi, mambo haya yananufaisha Kundi Moja lililo nyuma ya pazia na huku mambo yanapotifuka muhusika aliyechangia matokeo hayo anatoweka kama upepo na kuacha balaa limeanguka.

    ReplyDelete
  2. Wadau nisaidieni, cheo cha "Kamanda wa vyuo vikuu nchini" kimeanza lini, maana yake nini na shughuli zake ni zipi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...