Waendesha pikipiki zinazopakia abiria maarufu kama Boda Boda wako juu ya sheria na hakuna mtu anayeweza kutia fyoko, Globu ya Jamii inaweza kuthibitisha. Waendesha Boda Boda jijini Dar es salaam na hata mikoani wameanzisha himaya yao inayoonesha hata vyombo vya dola havina ubavu kuidhibiti, hata kama ni kuchukua sheria mikononi watakavyo na kuvunja sheria za usalama barabarani. 

Wananchi wengi tuliowahoji wametahadharisha kwamba endapo vyombo vya dola vitaruhusu hali hii iendelee, usalama na amani nchini vinaweza kuwa rehani kimoja. Wamehoji kwa nini hawa waendesha BodaBoda wamekuwa wajeuri na wababe dhidi ya wananchi tena mbele ya dola? "Bwana mwandishi ka ma unabisha hebu mgonge kwa gari Bodaboda mmoja uone jioni wenzie toka kila kona watakavyokutanika na kukushambulia na kukudhuru", anasema Mwananchi mmoja, akiendelea kushangaa pale Bodaboda wanapoachiwa kuvuka wakati taa za barabarani kuwa nyekundu. 

Globu ya Jamii jana Jumapili ilishuhudia Bodaboda wakitawala barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam wakati wakisindikiza gari linalosadikiwa kuwa na mwili wa mwenzao aliyefariki dunia, akipelekwa maeneo ya Ukonga kwa maziko. Kwenye makutano ya njia inayoelekea Uwanja wa Ndege wa kimataifa ya Julius Nyerere, ambapo pana taa za barabarani, umati huo wa Bodaboda ulifanya ubabe kupita wakati taa zilikuwa zinawaka nyekundu na hata askari trafiki aliyekuwepo pale alidharauliwa na badala yake mmoja wao ndio akawa anaongoza magari. 

Pia Daladala moja lililojaa abiria  lililazimishwa kibabe na kwa matusi kupaki pembeni ili msafara wa Bodaboda upite, na dereva alipotaka kungoja taa ziwake za kijani ili aendelee akazingirwa na Bodaboda kibao hadi akasalimu amri. Hali hii inazidisha maswali kwani hawa watu ni kina nani wafanye watakacho bila kujali sheria halali za nchi? 

Wananchi wametoa wito kwa wahusika kutathmini hali hii ambayo wameitaja kama bomu linalofukuta, na kisha kuchukua hatua haraka sana kabla hali haijawa mbaya zaidi ya ilivyo sasa. Vile vile wameshauri kuwepo namna ya kuwaelimisha Bodaboda namna bora ya kuendesha shughuli zao kwani kwa mfano mdogo tu wengi hawana utaalanmu wa kuendesha pikipiki, hali inayopelelea kukuta majeruhi wengi katika hospitali zote hivis sasa ni Bodaboda. 

"Hawa wanahitaji elimu ya namna ya kuendesha pikipiki ama sivyo tutapoteza vijana wetu kila siku" kasema mwananchi mwingine, akitolea mfano wodi ya Sewa Haji ya Taasisi ya Mifupa (MOI) iliyoko Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo kwa uchache tu waendesha Bodaboda 15 hulazwa pale kwa majeraha kwa siku.
Bodaboda wakiteka barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam
Mpita njia amepigwa butwaa kuona Bodaboda wanalazimisha Daladala lipaki pembeni ili wao wapite
Wengi ni vijana wadogo wa umri kati ya miaka 15 na 30.
Daladala likilazimishwa kupaki pembeni
Abiria wanashangaa kuona Bodaboda wakifanya watakalo
Gari walilokuwa wanalisindikiza likipita
Daladala limezingirwa na Bodaboda
Mmoja wa waendesha Bodaboda akielekeza pikipiki zipite huku daladala likiwa limesalimu amri na kupaki pembeni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hapa UK baiskeli zina njia zake, mabasi pia yana njia zake. Pia mtembea kwa miguu anapewa kipa umbele wakati wa kukata barabara.

    ReplyDelete
  2. tusipoziba ufa tutajenga ukuta! Nasema hivi hizi boda boda zote ziwe SCRAP yaani utaratibu huu wa usafiri uwe ni wa mtu binafsi na si wa biashara, vijiwe vyote vivunje . Waheshimiwa mnaotuongoza msipoliangalia hili kuna siku hawa jamaa watakuja kwa maelfu na hizo risasi zinazowalinda zitashindwa kufyatuliwa waje wawatoe kwenye viti vyenu vya ENZI. Hivi wakijikusanya vijana elfu 1000 na pikipiki zao kuja ikulu kufanya fujo mtawaweza?! Jiangalieni tena jiangalieni kwa sana sitoshangaa kusikia kuna vvikundi vya kigaidi kupitia kivuli cha bodaboda na hawa wanaojifua sikuhizi kwa madai ya kujiweka fit kila weekend asubuhi kuweni macho CCM!

    ReplyDelete
  3. ni kweli,hawa jamaa kama tutaendelea kuwachekea wataunda jeshi lao.

    ReplyDelete
  4. Na hapo hatujaruhusu bange.....

    ReplyDelete
  5. Hawa Polisi naona wamewashindwa kabisa hawa jamaa. Hii inaleta wasiwasi tunakoelekea kama utii wa sheria bila shuruti unaopigiwa debe unaweza fanikiwa nchi hii.Inabidi watu walazimishwe kuelewa kuwa hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria.Bila kupambana na wapindisha sheria kwa makusudi namna hii hatutakuwa na amani kabisa nchii hii, kwani inajengeka polepole tabia ya kuvuzivunja tena hadharani mwisho wa siku yatafanyika makubwa na hakutakuwa na wa kuzuia.

    ReplyDelete
  6. Lazima tujiulize vijana hawa nguvu na ubabe wanatoa wapi? Hilo picha hapo dogo!wameshawahi kuwasha moto hiace maeneo ya makonde mbezi beach.wameshawahi kuvamia kituo kidogo cha polisi kudai wapewe mtuhumiwa wamfundishe adabu!Tusibaki tunalaumu serikali hili lipo mikononi mwa vyombo vya dola (polisi).Hakuna bodaboda inayoruhusiwa kufanyabiashara bila dereva mwenye leseni.Khaa jamani hata hili tunafeli!!

    ReplyDelete
  7. nilichogundua ni kwamba hizo bodaboda nyingi ni za askari polisi ndio maana wanajiona wako juu ya sheria!!!!! huku mwanza kuna dada kapata ajali na bodaboda tena bodaboda ndie aliyejigonga kwenye gari ya huyo dada, yaani nusura wamtoe roho, walitaka kulipindulia gari mtaroni wakashindwa waka vunjavunja kioo cha mbele ili wamtoe wamuue, kwa bahati tukafika na askari ndio ikawa salama yake, ila sasa, aliyekua anaendesha ni day waka hana leseni lakini bado polisi wanamtisha huyo dada ili atoe rushwa kesi isiende mahakamani awalipe fidia kienyeji kwani wanajua wakienda mahakamani watashindwa!!!! hili ni bomu linalofutuka jamani mamlaka husika iliangalie hili kabla hatufika mbali

    ReplyDelete
  8. "Lazima tujiulize vijana hawa nguvu na ubabe wanatoa wapi?" Umasikini wa kufikiri.

    Wanajidai kujua haki; mbona wasipewe adhabu kwa kuendesha bila kuvaa helmets?

    ReplyDelete
  9. Hawa vijana noma...na ukizingatia wengi hawana elimu, wengine hawajaenda shule kabisa, wengine ni watoto chini ya 18. Sasa hebu fikiria fikra zao zikoje? ogopa mtu ambaye hana elimu.Maamuzi yake utachika mwenyewe. Nao wanajijua. Ukimgusa mmojawao hata kama yeye ndio mwenye kosa, hilo hawalielewi. Wao ni kushambulia tu.

    Sasa ona hata askari ameshindwa...Subirini sasa kitakachofuata..Hizi boda ni za viongozi. Nao boda cyclists wana jeuri kwa sabb wanaendesha boda za viongozi.

    Ukiona mtu yeyote analeta jeuri, ujue kuna mzito nyuma yake. Nashangaa wanaojiuliza kuwa hawa bodas jeuri wanalitoa wapi

    ReplyDelete
  10. Bange na Viroba jamani na sio akili zao.

    ReplyDelete
  11. Chezeeni hili bomu litakapolipuka ndio mtajua pumba na chenga ni zipi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...