Globu ya Jamii imepokea kwa mshituko mkubwa na simanzi taarifa kuwa Bi Kidude katutoka. Tunatoa salaam za rambirambi kwa watu wote wa Zanzibar pamoja na wa Bara waliomuenzi msanii huyu ambaye pamoja na umri wake mkubwa aliendelea kutuliwaza kwa usanii wake jukwaani pamoja na matani na ucheshi usio kikomo nje ya jukwaa. Kuna wachache wa aina yake Wallahi..
Akiwa ni mmoja wa wasanii nguli Bara na Visiwani, Bi Kidude alikuwa karibu sana na Globu ya Jamii kiasi ya kwamba pamoja na umri wake mkubwa, mara kadhaa alikuwa anatutia moyo wa kuendeleza libeneke kwa namna ambayo haitoweza kusahaulika. 
Alikuwa mtu wa karibu sana na Ankal, ambaye hata katika hali yake ya kudhoofu kutokana na umri na maradhi hakukosa kumtambua na kumtania. Ankal ni mmoja wa wanaLibeneke wachache ambao Bi Kidude aliwakubalia kupozi kupigwa picha nao.
Ni kweli kwamba kila mtu ataonja mauti, lakini si uwongo kwamba kuondokewa na kipenzi chetu Bi Kidude ni pigo kubwa kwa Globu ya Jamii kama ilivyo kwa jamii yote ya tasnia ya sanaa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MOLA AIWEKA MAHALA PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU BI KIDUDE
AMEN 
Picha ambayo Bi Kidude alimruhusu Ankal kumpiga
kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ankal samahani si vizuri kuuliza swali hili hapa ila naomba uniruhusu niliulize.Jina Kidude lilikuwa jina la kimuziki au ndilo haswaa jina lake halisi??Mimi nilidhani jina Kidude alilibuni mwenye kwa ajili ya shughuli zake za uimbaji kama wanavyofanya wanamuziki wengi duniani.RIP Bi Kidude

    David V

    ReplyDelete
  2. Inashangaza sana, huyu mama mbona hakupelekwa India au SA? What is the criteria of sending Tanzanians to India? She deserved to be looked after just like any other citizen. We are sending highly paid politians and bureacrats and forgetting the poor citizens.

    ReplyDelete
  3. Anony wa pili napenda nikuulize, kwani angepelekwa india ndo indefanya asife?

    ReplyDelete
  4. Shukran mtoa comment wa juu kuhusu kupelekwa nje. AGE na wakti. Alhamdulillah bibi yetu kafikia umri huo ambao ni wachache sana wataufikia. Mungu amlaze mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  5. Lakini hakuhudumiwa na wasanii wenzake kama ilivyoelezwa siku za nyuma .Leo mnamlilia..wasanii hebu tumia umoja wenu kusaidiana wakati wa haja

    ReplyDelete
  6. Mdau unaetaka apelekwe India, Bi Kidude alikuwa ana miaka zaidi ya 100, anasema alizaliwa enzi za Rupia, sasa tafakuri Rupia ilitumika miaka gani, then pata jibu na ukisikia amefariki shukuru AlhamduliLLAh amefika hapo je sisi tutafika huko ? Allah ampumzishe bibi wa watu, watu wamechuma sana kwa kumpitia mwache apumzike, maana mwisho walimfanya kama katuni !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...