Jeshi la polisi mkoani hapa limemtia mbaroni mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mhe Godless Lema kwa tuhuma za uchochezi kwa wanafunzi kwenye chuo cha uhasibu mwanzoni mwa wiki katika vurugu zilizotokea chuoni hapo baada ya mwenzao kuuwawa juzi usiku huko maeneo ya njiro jijini hapa
Kamanda wa polisi mkoani hapa kamishna msaidizi wa polisi Liberatus Sabas alisema kuwa Mhe Lema alikamatwa huko nyumbani kwake Njiro majira ya saa 9 usiku.
Afande Sabas alisema jeshi hilo linaendelea na mahojiano na mtuhumiwa na kuwa katika tukio hilo zaidi ya watuhumiwa 14 walifikishwa mahakamani jana na kuwa hao hawezi kuwaongelea kwani kesi yao ipo kwenye chombo hicho cha sheria.
Pia kamanda Sabas alisema kuwa Mh Lema anashikiliwa kutokana na vurugu zilizotokea juzi kwenye chuo cha uhasibu na kuwa atafikishwa mahakamani siku ya jumatatu.
Kwa upande mwengine Kamanda Sabas alisema kuwa zaidi ya hao watu 14 na Mhe. Lema hakuna mtuhumiwa mwingine aliyakamatwa. Awali ilisemakana wakili wake Albert Msando nae amekamatwa.
Mnamo siku ya Jumatatu mwanafunzi mmoja aliuwawa kwenye mitaa ya Njiro jijini Arusha na watu wasiojulikana hali iliyoleta tafrani hadi wanafunzi hao walipoleta vurugu chuoni hapo na polisi kutumia mabomo ya machozi kuwatawanya.
Sekeseke hilo lilimalizwa na jeshi la polisi baada ya wanafunzi kutotii amri ya mkuu wa mkoa huo Magessa Mulongo na kuanza kuingia barabarani kuandamana.
Wanafunzi Arusha zingatieni Masomo achene harakati za Kisiasa na kutimiwa vibaya Kisiasa na Wanasiasa huku mkiwa hamjijui!
ReplyDeleteHebu angalienei Mwanasiasa anashindwa kufikia malengo yake Kisiasa kwa njia sahihi za Kisiasa anakuja Chuoni anawadanganya ninyi Wanafunzi na kuwatumia vibaya ili afikie malengo yake kwa njia ya mkato.
Zinagtieni Masomo na Taaluma zenu kwa:
1.Kufanya Tafiti (Research and Development R&D ) ktk Mitaala na Fani zenu za Masomo badala ya kupoteza muda wenu wenye thamani kuwatumikia Wanasiasa walioshindwa ktk Uenezi na Sera za Kisiasa.
2.Mtumie muda wenu mwingi kwa Personal Developments and Group Developments with Capacity Building, badala ya Mandamano yasioyo na faida kwenu na kwa jamii.
3.Kutambua kuwa pana tofauti kubwa sana kati ya HARAKATI ZA SIASA ZA KIUPINZANI na UVUNJAJI WA SHERIA ZA NCHI!
TIME IS MONEY!
TIME IS LIFE!
Pole, you are really anonymous even your thinking! Wake up kamanda! If you real mean development when say develolment, then ignore your comments!
ReplyDeleteBahati mbaya umepoteza muda kuelezea kile ambacho wanafunzi wanakifahamu, hawa wanafanya wanachokijua na usidhani ni mbumbumbu wanaotumiwa na wanasiasa. Waache wadai wakitakacho kama ni nasomo watasoma tu hata hivyo mwisho wa siku ni wao watakaovuna na siyo wewe mpoteza muda kwa porojo nyingi zisizo na maana
ReplyDeleteHawa wa-Bunge uchwara, waache ubabe wa kilevi mitaani!
ReplyDeleteMdau wa kwanza kama unadhani labda kukamatwa kwa huyu mbunge kulikua ktk harakati zake binafsi basi utakua umetereza,si vibaya kuwashauri mema wanafunzi,ila soma magazeti ujue kikubwa alichokifanya mbunge siku ya tukio kisha ndio utoe maoni yaliyo sahihi.Magazeti yanatuambia hakuna baya alilolifanya zaidi ya kuwatuliza wanafunzi wasiende mbali zaidi.
ReplyDeleteNapenda kumuunga mkono mdau wa kwanza kabisa pale juu kabisa. Migomo kama hiyo ya kufuata mtu/ watu wenye kudanganya haiwasaidii. Msiwe kama kondoo mmoja akiwaambia basi nanyi mnafuata tu bila ya kuzingatia hoja muhimu na nini kimewaleta hapo shuleni. Kumbukeni kuwa mmeshika kwenye makali the end of the day you will be losers. Pigeni kitabu ndugu zangu acheni migomo isiyo na faida kwenu. Na kumbukeni kuwa hata kama kuna kitu ambacho hamkipendi hapo chuoni basi mfuate taratibu zinazokubalika na sheria za nchi au jamii kutatua .Kalenga boy
ReplyDelete