Hivi karibuni,kamera ya Globu ya Jamii ilimnasa mtu huyu anaedaiwa kuwa ni omba omba akiwa amekaa katikati ya Barabara ya Bagamoyo katika eneo la Victoria jijini Dar es Salaam,akijaribu kuomba wenye magari wanaotumia njia hiyo.hali hii ni ya hatari sana kwake,hasa ukizingatia kuwa barabara hiyo iko na njia tatu.
Home
Unlabelled
hii ni hatari sana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kweli ni hatari!! Lakini tunawaondoaje hao? Ile njia aliyotumia mzee makamba enzi zile kuwapakia kwenye mabasi na kuwarudisha makwao ni sahihi? Mbona wamezidi kuongezeka? Tulitafakari hili kwa kina kama taifa, tusiweke itikadi.
ReplyDeleteNashukuru sana kwa kututumia angalizo hili; mimi nimekuwa kila mara nikipita maeneo ya kuanzia Namanga kule kushuka hadi red cross pale utakuta kuna ombaomba wengi wanaingia barabarani huku magari yanapita, na cha ajabu unakuta kuna traffic pembeni anaangalia na wala hachukui hatua yoyote ya kuwatoa wale ombaomba; au inakuwa siyo kazi ya traffic? ni hatari sana. Na kama siyo kazi ya Traffic, basi wahusika wachukue tahadhari kwa hili swala.
ReplyDeletewatu hawana matumaini kwa hiyo kukaa kwenye barabara ni sawa na kutokaa kwenye barabara. Mtu anaona bora nihangaike kihivi na kigongwa na gari ni sawa tu.
ReplyDeleteUncle michuzi huyo ni wa siku nyingi sana,me pale namwona sasa mwaka wa tatu toka nifike dar.
ReplyDeleteAkiketi hapo bilakupata kitu kutwa nzima ataelewa kuwa hapafai, dawa ni kutompa chochote maana taasisi husika zimelala au goigoi.
ReplyDelete