African Women Entreprenuership Programme (AWEP) Tanzania Chapter imezinduliwa rasmi Ijumaa jioni katika hoteli ya Double Tree,mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Viwanda na Biashara ,Abdallah Kigoda ,pamoja na Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt

Hii ni Ngao iliyobidhiwa rasmi na Sylvia Banda ambaye ni balozi na mwenyekiti wa AWEP Zambia ,kudhihirisha kuwa AWEP Tanzania imezinduliwa rasmi kwa kuikabidhi kwa Mgeni rasmi wa Waziri wa Viwanda na Biashara ,Abdallah Kigoda na Balozi wa Marekani nchini ,Alfonso Lenhardt
Madam Sylvia Banza, Balozi wa AWEP Zambia akiikabidhi ngao hii , ambayo nae alikabidhiwa na Mama Bill Clinton alipoizindua AWEP Zambia mwaka juzi
Mwenyekiti wa AWEP Tanzania, Bi Flotea Masawe.
Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt, ambao ni wafadhili wa AWEP katika mkakati wake wa kuwakwamua wanawake wajasiriamali wa Afrika
Waziri Abdallah Kigoda akiwasili katika hafla ilofanyika jioni hii, na kuhudhuriwa na wanachama kutoka sehemu mbalimbali nchini, ambao baadhi walikuwa katika mafunzo ya kujifunza ujasiri amali ambao unalengo la kuwafanya wawekezaji
![]() |
Mama Lowasa pamoja na Balozi Maajar walihudhuria uzinduzi huu wa AWEP Tanzania |
Baadhi ya wanachama wa AWEP Tanzania Chapter katika picha ya pamoja na mgeni rasmi sambamba na Balozi Alfonso
burudani ilikuwa toka kwa Makumbusho Traditional Dancers
Picha na Shamim Zeze
Picha na Shamim Zeze
Wajasiriamali wanawake wa Kitanzania
waliowahi kushiriki katika Programu ya Wajasiriamali Wanawake wa Kiafrika
inayoendeshwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani wameanzisha tawi la
Tanzania la Chama cha Wajasiriamali Wanawake wa Afrika (AWEP). Tawi hilo limezinduliwa
leo katika hoteli ya Doubletree, Hilton jijini Dar es Salaam katika hafla
iliyohudhuriwa na Balozi wa Marekani Alfonso E. Lenhardt na Waziri wa Viwanda
na Biashara Dk. Abdallah Kigoda.
Katika hotuba yake wakati wa
hafla hii, Balozi Lenhardt alisema, "Kuzinduliwa kwa tawi la Tanzania la AWEP
kunaanzisha rasilimali muhimu kwa wajasiriamali wanawake nchini kote. Hivi sasa
wanawake wajasiriamali nchini Tanzania watakuwa na chombo watakachoweza
kukitumia kubadilishana mawazo na uzoefu wao kuhusu mbinu bora za kuanzisha na
kuendesha biashara. Balozi Lenhardt alisisitiza kuwa " Tawi la Tanzania la
AWEP ni kielelezo cha dhamira na jitihada za wanawake wa Tanzania za kuwajengea
uwezo wanawake wenzao nchini. Tawi hili litakuwa ni mtandao mwingine wa kukuza
sekta binafsi nchini na kuwasaidia wajasiriamali wanawake kutimiza ndoto zao."
AWEP ilianzishwa mwaka 2012
na washiriki wa Programu ya kila mwaka
ya Wajasiriamali Wanawake wa Kiafrika inayoendeshwa na Wizara ya Mambo ya Nje
ya Marekani kama hatua ya kwanza ya mkakati wa kujenga mtandao wa wajasiriamali
wanawake kutoka nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara waliodhamiria
kubadilisha jamii zao kwa kumiliki na kuendesha biashara ndogo ndogo na za kati
na kuwa sauti ya kuchagiza mabadiliko ya kijamii katika jamii hizo.
Msemaji wa Ubalozi wa
Marekani Bi. Dana Banks alisema, " Hadi mwishoni mwa mwaka huu ambapo
awamu ya tatu ya ziara za mafunzo nchini Marekani itakapokuwa imekamilika,
jumla ya wanawake wajasiriamali 122 wanaojihusisha na biashara ndogo na za kati
katika kilimo, usindikaji vyakula, mavazi, ubunifu, mapambo ya nyumbani na
sekta nyinginezo watakuwa wamehudhuria program ya AWEP."
AWEP ni programu ya Wizara ya
Mambo ya Nje ya Marekani inayolenga kuinua usawa wa kijinsia kwa kuongeza
ushiriki wa wanawake wa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika
shughuli za kijamii na kiuchumi. Aidha, programu hii inalenga kujenga mtandao
wa wajasiriamali wanawake katika nchi
hizo waliodhamiria kuchangia kuleta mabadiliko ya kijamii, ukuaji uchumi na
kupanua ukubwa na wigo wa biashara kikanda na kimataifa, hususan kuongeza
biashara na Marekani kupitia mpago wa AGOA.
Mwenyekiti wa tawi la Tanzania
la AWEP Bi. Flotea Massawe alisema "tawi hili litajenga mwamko wa wanawake
wa Kitanzania na kuwawezesha kubadilishana uzoefu wao. Aidha, litawapatia
nyenzo na fursa za kuwa viongozi katika jamii zao kwa kusukuma mbele gurudumu
la maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika jamii zao na kuwawezesha kuwa sauti
ya mabadiliko."
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...