Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma,Deusdedit Nsimek akionyesha nyara za serikali (mikia ya tembo) zilizokamatwa na Jeshi la Polisi MKoani humo.
Nyara za Serikali ambazo zimekamatwa(mikia kumi ya tembo)

Na Demasho Blog.

Jeshi la Polisi mkoa wa Ruvuma linamshikiria kijana ambaye anafahamika kwa jina la Bakari Said mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mkazi wa eneo la Mbalikiwa kata ya Ligunga Wilayani Tunduru kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali (mikia ya tembo).

Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma,Deusidedit Nsimeki ameyasema hayo leo mapema wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema jumla ya mikia ya Tembo 10 imekamatwa na askari ambao walikuwa doria katika eneo la Mbalikiwa mnamo tarehe Aprili 5, 2013 majira ya saa:7 usiku ambapo jumla ya idadi hiyo ya mikia ni sawa na idadi ya Tembo 10 waliouwawa na idadi ya meno ni 20 yenye jumla ya dola za kimarekani elfu 15 sawa na zaidi ya milioni 245 kwa fedha za kitanzania.

Mtuhumiwa Bakari Said leo alifikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kujihusisha na biashara hiyo haramu ya nyara za serikali ambapo taharifa ya tukio hilo la uhalifu zilipatikana kutoka kwa raia wema pia kamanda wa polisi aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wao wa dhati ili kuweza kudhibiti kabisa huarifu huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ivi mikia ya tembo ndio inafanana na nyaya kama hivi ktk picha??du kumbe.

    ReplyDelete
  2. Ebooo!

    Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni!

    Hivi mikia ya Tembo ni kama waya za chuma?

    ReplyDelete
  3. jamani ni macho yangu hii mikia mbona sielewe elewi?

    ReplyDelete
  4. Hiyo ni mikia kweli, Mbona inafanana na waya?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...