Ujenzi wa upanuzi wa barabara wa mwendo kasi katika ya barabara ya Morogoro ukiendelea katika eneo la Magomeni Mapipa, ujenzi huo utakapomalizika utarahisisha usafiri katika jiji la Dar es Salaam na kupunguza msongamano wa magari.
Ujasiramali upo wa aina nyingi ili kujisaidia katika kupata kipato na kuweza kujikimu . Pichani kijana akiwa amejiajiri kwa kazi ya kufuta vioo vya magari katika eneo la barabara ya Morocco jijini Dar es Salaam kama kamera yangu ilivyomnasa hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. huyo mteja tu, mimi nilimchukua na kumtunza na kutaka kumsomesha na pia nilimpa msingi wa biashara but matokeo yake akanikimbia na kuuza vyote nilompa na kurudia kazi hiyo ya kuomba na nilikua na mpango wa kuwatoa vijana kama hao but huyo kijana kanivunja moyo kabisa.
    mdau bigs london

    ReplyDelete
  2. Kaka hao vijana wengine ni wezi, wanajifanya kuosha kioo kumbe wanapiga taiming kwenye dash board kuna nini? Ukizubaa tu wamekuliza!!! Hao majanga tuulize sie.

    ReplyDelete
  3. Hawa vijana wa namna hii hawafugiki! hata wasichana wa kazi ni hivi hivi . Ukimpata aliyetoka sehemu ya vijijini ndani kabisa, akifika mjini tu miezi ya kwanza atafanya vizuri kama unavyomuelekeza. Lakini akishazoea , kama baada ya miezi 6 hivi, atarudia yale yale ya kwao. Usafi atajifanya hajui, kupika, hata tabia za kawaida tu zinakuwa hazifai.

    Hivyo hawa vijana ndio walivyo. Usije ukarogwa ukmachukua mtoto wa omba omba pale faya ukasema utakaa naye....uakiona cha moto. Hawa waacheni wakae hivi hivi.

    ReplyDelete
  4. Huo ujasiliamali unatia shaka, hiyo "wiper" aliyoshika ameipata wapi kama sio kuiba?

    ReplyDelete
  5. hao watoto ni timed bomb, ni wezi balaa, wasiposhughulikiwa hatima yao watakuja kuwa majambazi wazoefu!

    ReplyDelete
  6. Majambazi sugu wa kesho hao mnawalea kwa kuwapa Tsh 200 zitawatokea puani.Maana mtoto alievuta bangi, petrol anatukana hovyo kumpa hela sio msaada.

    ReplyDelete
  7. anayefutiwa kioo naye pia aliingia mjini kwa kuzuga mtaani ndio maana anasupport ujinga. anaefuta na anaefutiwa wote sawa tu

    ReplyDelete
  8. Ni kweli ni weze na tabia zao ni mbaya lakini kama mkitaka kuwasaidia muwapeleke rehab kwanza so mnawachukua tu na kuwabwaga kwenye maisha ya palace wakat walishazoea utaratibu wa kwao.

    ReplyDelete
  9. Wadau wamefanya kazi nzuri sana kutoa maoni yao, yote yana uzito wa kufanyiwa kazi na SERIKALI. Naomba wahusika mlishughulikie suala hili haraka iwezekanavyo ili nchi yetu iendelee kuwa na AMANI kwa kuwa na raia wema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...