Mhe. Sophia Simba akipewa maelezo na Bill Marwa kuhusiana na  tovuti rasmi iliyotengenezwa maalumu kwa ajili ya kupaza sauti ya mwanamke (www.sautiyamwanamke.org) baada ya kuizinduwa kwenye uzinduzi wa Mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake unaofanyika Dodoma.  Waliosimama kushoto kwa waziri ni Teresa Yates na Hilda Mashauri viongozi wa mtandao wa jinsia wa asasi za kiraia (CSO Gender Coalition) waandaaji wa mdahalo huo.Tovuti hiyo itatumika kutoa taarifa za kila siku za mdahalo na kuendelea kupaza sauti ya mwanamke baada ya mdahalo kwa kuandika habari mbalimbali zinazohusu mwanamke. 
Teresa Yates, Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania akikabidhi zawadi kwa Mhe. Sophia Simba (MB) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na Watoto  na kwa Dr. Rose Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. 
 Mwanahamisi Salim, Meneja wa Kampeni, Ushawishi na Utekelezaji wa Haki za Kiuchumi kutoka shirika la Oxfam akiendesha zoezi la ufunguzi wa Mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake unaofanyika katika ukumbi wa Chimwaga Mjini Dodoma. 
 Dr. Rehema Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akimkaribisha mgeni rasmi Mhe. Sophia Simba (MB) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na Watoto kwa ajili ya kufungua rasmi mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake. 
  Mshiriki kutoka Unguja akizungumza kwa niaba ya wanawake takribani 300 wanaoshiriki mdahalo wa kitaifa wa wanawake uliozinduliwa leo Dodoma na Mhe. Sophia Simba (MB) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na Watoto. 
  Baadhi ya Wanawake wanaoshiriki Mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake. Mdahalo wa Kitaifa wa wanawake ni tukio linalofanyika kwa hisani ya mtandao wa jinsia wa asasi za kiraia (CSO Gender Coalition) kuanzia tarehe 10-14 April, 2013 mkoani Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mashallah nimependa sana jinsi unavyojistiri umefunika kichwa chako ndio ustaarabu japo kifua kipo wazi inshallah mola atakungoza kesho ujistiri na kifua

    ReplyDelete
  2. Hii midaalo mnayosema ni ya wanawake , ni wanawake wa aina gani mbona wengine hatuna habari? Kama ni wanawake wote tangazeni : tv , magazetini n.k ili anayetaka kuja aje kama ni kuchangia. Hapa unaweza kuta ni wake wa vigogo, watoto wao, wajukuu,wakamwana, mawifi na wakwe

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli Midahalo ikome. Sasa ni saa za Kazi za vitendo. Tumedahalo ya kutosha tangu 1975 UN Women Conference in Nairobi, 1995 Beijing.... Yameandikwa na yanazidi kutafitiwa na kuandiwa masuala ya wanawake na jinsia. Tuyatafute, tusome, tuyafanyie kazi. Moja ni huu Msiba wa elimu. Tunahitaji kudahalo kwa nini Binti zetu hawafaulu kweli? au hawapo hapsaaa katika Science na Hesabu? Tuanche kulemazika na Bahasha za wafadhili. Hawa wako kazini nanyi nyiyo kitega uchumi chao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...