Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 na mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa Fedha 2013/2014 kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (hawapo pichani) inayoongozwa na Mhe. Edward N. Lowassa (Mb.) (kulia). Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam leo 
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe (hayupo pichani).


Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wengine wa Kamati hiyo wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (kulia-mstari wa kwanza), akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa kikao kati ya Uongozi wa Wizara na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Wengine katika picha ni Bw. John  Haule (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Rajabu Gamaha (kushoto), Naibu Katibu Mkuu.

Baadhi ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa kikao kati ya Uongozi wa Wizara na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Wakurugenzi wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani).

Wakurugenzi na Wajumbe wengine kutoka Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Waziri Membe (hayupo pichani) wakati wa kikao kati ya uongozi wa Wizara na Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...