Mganga Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Dk Salum Rashid Kabuma, akitoa tathmini ya jinsi mkoa huo ulivyojipanga kukabiliana na Afya ya Uzazi wa mtoto, baba, na mama katika kukabiliana na maambukizi mapya ya VVU mbele ya ujumbe kutoka Vodacom Foundation na Taasisi inayojishughulisha na afya ya uzazi ya EGPAF (hawako pichani) uliofanya ziara ofisini kwake. Vodacom hivi karibuni ilichangia mashine 8 za kisasa ‘sms printers’ zenye thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekani elfu 10 zinazowezesha upimaji na upatikanaji wa majibu ya VVU kwa watoto wachanga kwa haraka wanaozaliwa mkoani humo.
Mratibu wa Uchunguzi wa VVU kwa Watoto Wachanga wa EGPAF, Georgiah Kasori, (kulia) akipewa maelezo na Meneja wa Maabara wa mkoa wa Mtwara, Joachim Mrope ya jinsi mashine ‘sms printer’ zinazowezesha upimaji na upatikanaji wa majibu ya VVU kwa haraka kwa watoto wachanga zinavyofanya kazi kwenye maabara ya hospitali hiyo jana.
Meneja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon, (kushoto) akiagana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Dk Salum Kabuma, baada ya kupata taarifa fupi ya maendeleo ya Afya ya Uzazi wa Mtoto, baba na mama. Vodacom Foundation walikuwa katika ziara ya kuangalia maendeleo ya ufanisi wa mashine zake takriban 8 za kisasa zijulikanazo kama ‘sms printer’ walizozitoa mkoani humo hivi karibuni, kuwezesha upimaji na upatikanaji wa majibu ya VVU kwa haraka kwa watoto wachanga.
Katika hali isiyo ya kawaida kwa akinababa wengi nchini, mkazi wa Naliendele, mkoani Mtwara, Salum Abdalah, akihudhuria kliniki na mtoto wake, katika kituo cha afya cha Naliendele mkoani humo jana kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya afya ya mtoto, Zahanati hiyo ni miongoni mwa zilizonufaika na msaada wa mashine za kisasa ‘sms printers’ zinazowezesha mchakato wa upimaji na upatikanaji wa majibu ya VVU kwa haraka kwa watoto wachanga.
Akinamama wa mkoa wa Mtwara wakihudhuria kliniki ndani ya Hospitali ya Mkoa huo, kwa lengo la kuangalia maendeleo ya afya ya watoto wao. Vodacom Foundation walikuwa katika ziara ya kuangalia maendeleo ya ufanisi wa mashine zake takriban 8 za kisasa zijulikanazo kama ‘sms printer’ walizozitoa mkoani humo hivi karibuni, kuwezesha upimaji na upatikanaji wa majibu ya VVU kwa watoto wachanga kwa haraka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. VVU NI NINI?
    Mara nyingi mnaadika hivi vifupi bila kuweka kirefu chake hata mra moja katika taarifa nzima. Naomba mfuate kanuni za uandishi tafadhali.

    ReplyDelete
  2. Vijidudu Vya Ukimwi =VVU uwe update kama mimi!

    ReplyDelete
  3. Mdau 05:39 hauko mbali sana, ila VVU ni kirefu cha `Virusi Vya UKIMWI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...