MAREHEMU SARAH NELSON MAKINDA
Kwa kila jambo kuna majira yake na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu MHU 3:1
Ni mwaka mmoja leo tangu uitwe nyumbani Ingawa tupo mbali na wewe, lakini umetutoka kimwili tu, kiroho tuko na wewe. Bado tunakumbuka kauli zako, ushauri wako katika familia yako uliyoiacha katika wasiwasi mkubwa. Tumelia sana, Tumeumia sana lakini yote ni mapenzi ya Mungu
Kazi ya Mungu haina makosa, lakini kwetu ni majonzi makubwa.
Kama binadamu tungekuwa na uwezo wa kukata rufaa ya kifo, hakika nasi tungekata rufaa mbele ya Mungu ili turudishiwe Dada /mama yetu kipenzi, SARAH NELSON MAKINDA, na kuendelea kuishi pamoja nae hapaduniani.
Picha na mtiririko wa maisha yako ni ushahidi kuwa wewe ulikuwa dada/mama bora kwetu, huku tukiamini Mungu muweza na muumba wa yote ataitumia fursa hiyo kama sehemu ya kukulaza mahali pema kwa unyenyekevuwako.
Suala zima la kifo, linaashiria kuwa ni sehemu ya mpito katika maisha ya duniani. Vitabu vyote vya dini vimekitaja kifo kuwa hakuna kiumbe ambaye anaweza kuvuka bila kupitia katika hatua hiyo, hivyo tunatumia nafasi hii kukuombea mwanga na raha ya milele akuangazie na ulale mahali pema peponi.
Unakumbukwa sana na mtoto wako mpedwa Emaculata Mwasakyeni,baba yako mzee Nelson Makinda,dada yako Wende,wadogo zako Richard,Mariam.Daniel na Elizabeth,shemeji zako Joseph Mwigune,Geofrey Mlagha na Michael Mbwambo,wifi zako StahimilMsigwa,mama Emmy,mama Jackline na mama Mwasakyeni,familia yote ya Makinda,Magehema,Mwasakyeni na ndugu jamaa na marafiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...