Na. ELIPHACE MARWA
na FRANK SHIJA - MAELEZO
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar kaushiria Muungano uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miaka 49 iliyopita.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan ametoa
wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi kesho katika maadhimisho ya miaka 49
ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Ametoa kauli hiyo leo jijini
Dar es salaam wakati wa mkutano na waandishi wahabari kuzungumzia maadhimisho hayo
yatakayofanyika kesho katika uwanjwa wa
Uhuru jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa kesho ni
siku muhimu kwa Watanzania kuenzi na kuudumisha Muungano kwa kuwa umesababisha Tanzania kupata heshima
kubwa Afrika na duniani kote.
“Ninatoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kwa
wingi katika maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wetu, kwani hakuna asiyejua
kuwa Muungano huu umetuletea heshima kubwa kimataifa, hivyo ni wajibu wetu
kuulinda na kuudumisha” amesema Mh. Samia.
Aidha Waziri huyo amesema kuwa pamoja na changamoto
zilizopo Muungano umeendelea kuimarika kwa kuwa wananchi wana imani kubwa na
Muungano huu na Serikali imeendelea kushughulikia kero mbalimbali za Muungano.
Mh. Samia ameongeza
kuwa katika kushughukia kero zilizopo katika Muungano , Serikali ya awamu ya
tatu mwaka 2004 iliunda kamati yenye wajumbe kutoka pande mbili za Muungano ya
kushughulikia kero hizo.
Aidha,mwaka 2006 kamati
hiyo ilianza kushughulikia kero hizo
mpaka sasa jumla ya hoja tisa kati ya hoja 13 za Muungano zimekwisha kamilika
na kupatiwa ufumbuzi.
Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar uliasisiwa na Hayati Baba wa
Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume tangu tarehe
26/04/1964 ambapo kesho unatimiza miaka 49.
Mungano mzuri halafu mikamati tele ya kurekebisha kero. Sasa kinasherehekewa nini? Kero au Muungano?
ReplyDelete