Familia ya Kanumba inawakaribisha katika kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha marehemu Steven Kanumba itakayofanyika Leaders Club  Jumapili hii tarehe 7 /04/  2013 kuanzia saa 10 jioni.

Saa moja ya siku hiyo kutakuwa na uzinduzi wa muvi ya mwisho kufanywa na marehemu. Pia itaoneshwa kwa mara ya kwanza preview ya muvi iitwayo After death(Never happened before) iliyoandaliwa na Jackline Wolper kwa ajili ya kumuenzi marehemu Kanumba.Kutasindikizwa na burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na  wachekeshaji maarufu Tanzania.
KIINGILIO NI BURE. 
MSIKOSE TUMUENZI NDUGU YETU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. mimi sio mpenzi wa sinema za kitanzania lakini niliangalia juzi senema ya huyu jamaa kwakweli senema za tanzania ni boring sana

    yani wajamaa wananyata utasema nini wapo slowly sana mpaka unaboeka kuangalia

    alafu sasa kwa upande wa mafundisho ndio zero kabisa yani sijaona mafundisho ya maana kwa jamii

    maadili ni mabovu kabisa wanavaa nusu uchi wananyonyana midomo

    hivi hizi senema zinaendana na maadili ya kibantu kweli?
    hizi senema huwezi kuangalia na watoto wako ni aibu kubwa

    wanachafua mazingira ya familia sana hawa jamaa

    ningelikuwa kama ni mhusika wa serikali basi hizi senema ningekuwa nazipitia na kutoa viwango
    zisizofaa kwa jamii nisingeziruhusu kuonyeshwa.

    ReplyDelete
  2. Meandeleo yote ni kuiga magharibi baba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...