Serikali imeona kuzuka kwa tabia ya uvunjaji wa kanuni ya utunzaji wa siri za taarifa za mawasiliano binafsi ya watumiaji wa huduma za simu za mkononi. Taarifa hizo zimefikia hatua ya kuchapishwa katika vyombo vya habari kwa kutaja bila idhini yao, namba za simu, wahusika wa namba hizo, maongezi na muda wa mawasiliano Kati yao. Jambo hili ni Kosa la Jinai. 

Serekali inapenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha wenye makampuni ya Simu, Vyombo vya Habari na wananchi kwa ujumla kuwa, kutoa taarifa za mawasiliano binafsi ya simu baina ya watumiaji wa huduma hiyo, ni uvunjaji wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Na. 3 ya mwaka 2010 na Kanuni za Mawasiliano (Kulinda Wateja) za mwaka 2005.

Kifungu cha 98 ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kinasema;

“Mtu yeyote ambaye ni mfanyakazi wa kampuni yenye leseni ya kutoa huduma za mawasiliano, au mwakilishi wake, ana wajibu wa kutunza siri za mawasiliano binafsi na taarifa zozote za siri za wateja kwa mujibu wa sheria hii”. Aidha, “Mtu yeyote haruhusiwi kutoa taarifa binafsi za mteja yeyote alizopokea au kusikia kwa mujibu wa sheria hii isipokuwa tu mtu huyo ameruhusiwa kwa mujibu wa sheria”

Kanuni ya 12 ya Kanuni za Mawasiliano za mwaka 2005 za Tanzania (Kulinda Wateja) inasema:-

“Mtoa huduma za Mawasiliano haruhusiwa kuingilia kati, kusikiliza au kutoa taarifa zozote za mazungumzo ya mteja yeyote yaliyopitia kwenye mtandao wa mtoa huduma, isipokuwa kwa ruhusa kulingana na mahitaji maalumu kwa mujibu wa sheria zilizopo”

Hivyo basi wananchi wanapewa tahadhari kuhusu kutafuta au kutaka kupata taarifa za mawasiliano ya siri kutoka kwa watoa huduma na kuzitumia taarifa hizo binafsi za mawasiliano pasipo kufuata utaratibu ulioruhusiwa kisheria.

Aidha Serikali inapenda kuwatoa wananchi hofu kuwa Mawasiliano yao (maudhui) hayapaswi kuingiliwa kwa kusikilizwa mazungumzo yao au kusomwa meseji zao katika mitandao ya simu. Serikali Kwa kutumia vyombo vyake vya usalama inawahakikishia wananchi kuwa haki zao za faragha katika mawasiliano zinalindwa Kwa Mujibu Wa Sheria Na. 3 ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2010 pamoja Na Kanuni zake.

Kwa taarifa ambazo zimechapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari hivi karibuni, Mamlaka ya Mawasiliano pamoja na taasisi nyingine husika kwa mujibu wa Sheria ya EPOCA pamoja na Kanuni zake, wanaelekezwa kufanya uchunguzi wa uvunjwaji huo wa sheria na Mamlaka husika zichukue hatua za kisheria kwa yeyote atakayebainika kuvunja sheria hiyo. 

Serikali inayakumbusha Makampuni ya simu, Vyombo vya Habari na wananchi kwa ujumla kuhakikisha siri za mazungumzo binafsi ya wateja zinahifadhiwa na hazitolewi kwa yeyote isipokuwa kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Ni kweli kwa sababu always nikimpigia mzazi wangu simu yaani kuna watu wanasikiliza na hata text wanaziingilia .Nilishamfahamisha mzazi wangu na tulireport police,EEGH

    ReplyDelete
  2. Ikiwa kampuni iliyovunja sheria inajulikana. serikali imeisajili na kuipatia nakala ya kanuni za uendeshaji. kwa mawazo yangu njia sahihi ya kuikumbusha jamii ni kuichukulia hatua zinazofaa kampuni husika. mdau ukerewe

    ReplyDelete
  3. Watoto aw viongozi wastaafu na wasasa angalieni Mnavyoandika Facebook na simu zenu mbadilishe ikiwezekana .Twitter accounts zenu angalieni mnachopost.Mumer na private life,

    ReplyDelete
  4. Watoto wa viongozi muwe waangalifu mtajikuta text zenu email zimeanikwa.Maadui wengi sasa

    ReplyDelete
  5. Mimi hoja yangu moja tu Serikali ni yetu wote hivyo ifanye kazi kwa maslahi ya wote na wote tupate huduma kwa usawa

    ReplyDelete
  6. Ndiyo ni kweli lakini hii imekuja baada ya wanasheria kuwahusisha viongozi wa serikali katika kujua maozo yao.iruhusiwe kupatikana kwa txt messages za viongozi wanaokula rushwa na wanaopanga njama za uhaini katika nchi yetu.

    ReplyDelete
  7. kwa ulimwengu tunaoishi easy dropping ingetakiwa serikali ndio imehalalisha. mtu yeyote ndiyo unatakiwa kuwa mwaangalifu na kujua jinsi ya kutumia electronics. sasa kama ni wahalifu wanapanga jambo ina maana mtu atakayewasema atakua amevunja sheria?

    Hapa imekaa vibaya inaonekana serikali ianataka kuwalinda watu wao watakaokuwa wanapanga mishens kwenye vyombo vya habari.

    ReplyDelete
  8. Sio kweli ni wivu na chuki Za watu tu .chuki zimezidi sana ,umbea umbea tu

    ReplyDelete
  9. You need court order.watu Mna hack Facebook email Za watoto wa vigogo na wazazi Wao for what ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...