Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam, hatua ya sita bora imeanza jana Aprili 15 katika viwanja vitatu na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:
Uwanja wa Makurumla- Red Coast iliichapa Abajalo FC 1-0. Bao hilo lilifungwa na Rashid Juma.
Uwanja wa Airwing-Shariff Star iliifunga Boom FC 1-0.
Bao hilo lililifungwa na Mandewa Mrutu ‘Niyonzima’.
Uwanja wa Kinesi-Friends Rangers vs Day Break hazikufungana.
Ligi hiyo itaendelea Alhamisi, Aprili 18, ambapo Boom FC itacheza na Day Break, kwenye uwanja wa Airwing, wakati Friends Rangers wao watachuana na Red Coast kwenye uwanja wa Kinesi, huku Abajalo wakichuana na Sharif Stars kwenye uwanja wa Msasani.
Imetolewa na Mohamed Mharizo
Ofisa Habari Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...