NAIBU Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki amewataka
wanachama wa kikundi cha waandishi wa habari cha kujikomboa
kiuchumi (Habari Group) kupendana na kuaminiana ili kukifikisha
kikundi hicho mbali.
Kairuki ambaye pia ni mlezi wa Habari Group, alikitaka kikundi hicho
kutokuwa wachoyo wa kusaidia waandishi wa habari wengine wenye nia ya kuungana na kufanikiwa kimaisha, na kwamba ili mtu
afanikiwe ni lazima awe mwenye upendo na kusaidia wengine pale
penye mwanya wa kufanya hivyo na kuwataka wanachama wote kuwa na moyo wa kujitolea kwa ajili ya kikundi.
"Sitopenda kusikia kikundi hiki kimekufa kwa sababu ya mifarakano na chuki miongoni mwenu kwani kwa kufanya hivyo hamtofikia malengo mliyokusudia," alisema Kairuki.
Aliongeza kuwa wakati anaingia madarakani aliweka vipaumbele kwa wafanyakazi wa majumbani, madereva wa aina zote, wafanyakazi wa mashambani, wahudumu wa baa na nyumba za wageni, walinzi na waandishi wa habari.
Na kwamba ameanza kushughulikia haki mbalimbali za makundi hayo, ambapo kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kuishinikiza serikali kusaini mkataba wa kuridhia haki za wasichana wa majumbani.
Aliwapongeza waandishi wa habari kwamba pamoja na changamoto
nyingi wanazokutana nazo, lakini hawakati tamaa na wamekuwa
wakifanya kazi yao kwa moyo mmoja na kwa bidii.
Kama mkakati wake wa kuwasaidia waandishi wa habari, alisema
atasimamia Habari Group ili wawe mabalozi wazuri kwenye mambo
mbalimbali kwa jamii, ikiwemo kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali,
kuwapa elimu ya umuhimu wa cheti cha kuzaliwa, sambamba na
kushirikiana nao bega kwa bega kwenye mambo muhimu ya kijamii.
"Kuwasidia kwenu ni miongoni mwa malengo yangu niliyojiwekea ya
kupigania haki ya baadhi ya makundi ambyo nimeona haki zao kama wafanyakazi hazitekelezwi,"aliongeza.
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki, akiongea na kikundi cha wanahabari wanawake HABARI Group jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Jokate Mwegelo ambaye nid Dada Mlezi wa kikundi hicho
Mwanahabari akitoa maoni katika kikao hicho
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki akisikiliza maoni mbalimbali ya wanakikundi hao
Akibadilishana mawazo na wanakikundi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...