.jpg)
Kwanza kabisa napenda kukupongeza kwa kazi kubwa na nzuri ya kutuhabarisha,Ubarikiwe sana!
Brother,Nina aunt yangu mmoja ambaye kwa sasa ni zaidi ya miaka mitatu amekuwa akiishi kwa shida mateso na maumivu makali kupita maelezo, Huyu aunt amepatwa na uvimbe wa ajabu mguuni ambao ulianza kama uvimbe wa kawaida mfano wa mtu unapokuwa umekaa kwa muda mrefu ukiwa safarini.
Baada ya miezi kazaa mguu uliendelea kujaa kwa kasi ndipo akabidi aende KCMC HOSPITAL kwa ajili ya vipimo,ma daktari walifanya vipimo pamoja na elephantiasis(matende) lakini vipimo vyote vikaja negative ikabidi aanzishiwe dozi za anti biotic.
.jpg)
.jpg)
Brother,Naomba unipostie hii ili kama kuna mdau yeyote anaeweza kutusaidia kwa ushauri au njia yeyote yakupata ufumbuzi juu ya hili na zaidi kutibiwa tutashukuru sana, Nimeambatanisha picha za mguu jinsi ulivyo fikia kwa sasa.
Natanguliza shukran zangu za dhati
Mdau Shomari Mob: +255 779970000
Pole sana mgonjwa, na poleni familia kwa kuuguza, mi nilikua nafikiria labda kama ungeomba msaada wa mchango aende India kwa matibabu zaidi, hapa bongo kwetu kwa kweli ni shidaaa!
ReplyDeletempelekeni kwenye maombi kwa T B.JOSHUA atafunguliwa tu
ReplyDeleteasante
Hii ni lymphatic filariasis ambayo imeathiri miguu ama mguu yaani elephatiasis. Wadudu wanaosababisha ugonjwa huu wanaishi kwenye mfumo wa lymph ambako wanaziba mifereji yake inayoitwa lymphatics. Ukweli ni kwamba ikishafikia hatua hiyo haiwezi kutibiwa hata Marekani acha India na Muhimbili. Huo mguu hauwezi tena kurudi katika hali yake ya kawaida. Wadudu hawa pia wanaweza kusababisha kuharika kwa umbo ya nje la uke na kuwa kile kinachoitwa: Cauliflower vulva.
ReplyDeleteTatizo ni kwamba madaktari wetu hawana muda wa kukaa na wagonjwa na kuwaeleza vizuri nini kinaendelea katika miili yao. Nini kinawezekana na nini hakiwezani. Katika hali hiyo ya dada, kinachohitajika ni good personal hygiene. Usafi wa mwili kwa ujumla na hasa hiyo miguu. tatizo la miguu hiyo ni kwamba ni rahisi kupata maambukizo mengine ya bakteria. Kukiwa na maambukizo ya aina hiyo mgonjwa hupewa antibiotics. Na kwa maambukizo hayo mguu ulikuwa unatoka usaa. Na ni kwa sababu hiyo hiyo alipewa antibiotics. Hizo antibiotics si za kuurudisha mguu katika hali yake ya zamani.
Madaktari wenzangu, tupate muda wa kuwaelimisha wagonjwa wetu kuhusu yanayowasibu. Wagonjwa si wajinga, watatuelewa.