Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Tanzania Bw Damian Lubuva
--
Tume ya uchaguzi ya Tanzania imesema ina mipango ya kutumia mfumo wa kieletroniki kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 inatekelezwa.

Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari nchini Zimbabwe, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Tanzania Bw Damian Lubuva amesema serikali imetoa uamuzi huo ili kufanya mchakato wa upigaji kura uwe salama na kuongeza imani kuhusu usahihi wa matokeo ya uchaguzi. 

Bw Lubuva amesema kwa sasa serikali ya Tanzania inajiandaa kutoa zabuni ili kupata mfumo huo, lakini gharama zake bado hazijajulikana, lakini wataomba wahisani kugharamia mfumo huo. Bw Lubuva pia amekanusha habari kuwa kuna usiri kwenye mchakato wa kupata mfumo huo. 

Tume ya uchaguzi ya Kenya ilitumia mfumo huo kwenye uchaguzi mkuu uliopita lakini mfumo huo uliachwa kutokana na matatizo ya kiufundi
.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. not bad in the sense of development,,,but please people think about it,,,kwa wenzetu abao to think of it wako juu kidogo kenye IT,,this system didn't work,,don't you think hii ni plan B ya kuiba kura...hatakama watanzania hatujui enough but we can reason,,,so i think we shouldn't fall for that...at least that's what i think.

    ReplyDelete
  2. JAJI LUBUVA ushauri wangu ni kuwa 2015 ni jirani sana na huo mchakato wa kuweka hiyo system unahitaji miaka 10 ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na mafunzo kwa watumiaji na wataalamu.Kusema kuwa tunataka kutumia hiyo system 2015 ni kuwadanganya wananchi sababu watu wengi vijijini wanahitaji mafunzo ya jinsi ya kutumia hizo system iwe kompyuta au simu.Na ili kuwa fikia wananchi wote mpk maeneo ambayo hamna mawasiliano ya barabara na umeme inahitaji muda na si kukurupuka.hapa naona tume mnataka kuparamia treni kwa mbele bila kupata ushauri toka nchi ambazo walishaweka na kutumia kwa ukamilifu hii system.Tujipe muda wa miaka 10 mpk 2025.Infact hii tunaweza iweka kwenye vision 2025.

    ReplyDelete
  3. Hii System haitafanya kazi vizuri 2015. Ukiiga tembo kunya utapasuka msamba. Tusubiri miaka ya mbele sio 2015.

    ReplyDelete
  4. Mwenzio aklinyolewa na wewe tia maji!!!

    Hivi hatujifunzi makosa yaliyofanywa na jirani zetu Kenya mwezi uliopita?

    Kenya hiyo BVR (Biometric Voter Registration)imebuma, na wao wanajiweka mwbele kwamba wapo vizuri ktk mwamko wa matumizi ya IT,sembuse iwe sisi?

    Kama mnavyoona Kenya wameweza kuwashawishi Makampuni makubwa ya Marekani kama IBM,Microsoft, Google, Motorola, Macintosh na mengine ya nchi zingine kama Samsung na Nokia yaweke Makazi Nairobi Kenya kwa niaba ya Afrika nzima na Afrika ya Masharikina Kati, licha ya hivyo Mfumo umewabumia kama 'BUNDI ANAVYOMFIA MCHAWI MIKONONI'.

    Matokeo yake Mgombea Odinga anatumia udhaifu wa kushindwa kwa Mfumo wa IT ktk kufungua Kesi ya Pingamizi la Uraisi.

    Tuangalie kuimarisha Uwazi zaidi kwa kutumia Mfumo wa kawaida wa Kura (MANUAL) ni bora badala ya kuegemea Tekinolojia yeye uhakika wa utata.

    ReplyDelete
  5. Albert Einstein aliwahi kutoa maneno haya:

    ''“I fear the day when the technology overlaps with our humanity. The world will only have a generation of idiots.”
    ''

    -----------------------------------

    ''YAANI ''Ninaogopa siku matumizi ya mwanadamu ktk Tekinolojia yanapindukia dhidi ya utu wetu. Dunia itakuwa tu na kizazi cha Wajinga''

    -----------------------------------

    Ni wazi ya kuwa Albert Einstein alikuwa ni Mwanasayansi lakini hakupendelea matumizi kupita kiasi ya Sayansi na Tekinolojia kwa kuwa alitambua ya kuwa yana madhara makubwa, ni bora kutumia zaidi asilia !

    Ktk Mchakato wa Kura mwaka 2015, juu ya matumizi ya Sayansi na Tekinolojia tuzingatie maneno ya Mwanasayansi huyo wa Karne ya 19.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...