Mtoto Abdallah anasumbuliwa na tatizo la MOYO, Moyo wake ni Mkubwa, Kwa sasa Amelazwa Katika Wodi ya Watoto Katika Hospitali ya Mnazi mmoja, ambapo anaendelea kupata Matibabu lakini LENGO ni kusafirishwa Nje yaNchi. Pia Anasumbuliwa na Maradhi ya Tumbo Kujaa Maji ambapo analazimika Kutolewa Maji Kila Baada ya Siku 3.

Kwa Yoyote Anayeweza Kutoa Kiasi chochote Cha Msaada Unaweza Kutumia Namba hii 0774 64 87 80 kuwasiliana Mama Mzazi wa Abdallah.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Serikali impeleke India huyu kijana. Kodi zetu zinatumika kupeleka politicians na bureaucrats ambao wanalipwa mishahara mikubwa sana. Kwa nini huyu asisaidiwe?

    ReplyDelete
  2. Mtoto huyu hahitaji hata kuombewa msaada, hili ni jukumu la serikali moja kwa moja. kama inaweza kuwakimbiza kwa ndege nchi za nje wakubwa ambao matatizo yao yanatibika hapa nchini,kweli la malaika huyu ishindikane. Jamani hebu tuwe na mioyo ya huruma kwa wasio na kitu!!!!!

    ReplyDelete
  3. subahanallah; sasa viongozi wako wapi??? jamani; yani inashindikana milioni ishirini au hamsini ya kumpeleka huyu mtoto. HUMAN DIGNITY iko wapi hapo??? Ivi thamani ya binadamu ni kiasi gani? Nijuavyo miye ni kubwa sana; huwezi kulinganisha na kitu chochote. Viongozi wote watakuwa masuhuru mbele ya Aliyewaumba siku ya hisabu; wewe wafanye masihara tu.

    ReplyDelete
  4. serikari inatakiwa iwezeshe madaktari matibabu haya yafanyike hapa nyumbani tutapeleka watu india hadi lini? tubadilike jamani

    ReplyDelete
  5. JK ataiona kupitia Michuziblog!

    Wakati mwingine wazazi, msingoje dakika ya mwisho. Huo ugonjwa hao haukuanza jana!

    ReplyDelete
  6. Wizara ya Afya mko wapi? Mnapeleka watu kwa medical check ups tena wenye uwezo na case kama hii madaktari wanazembea kuileta Wizarani moja kwa moja? Kweli priorities za Madaktari wetu zinahitaji msaada.

    ReplyDelete
  7. ALLAH AKBAR... MWENYEZIMUNGU AKUTILIE WEPESI MDOGO WANGU UPONE NA WAUGUZI POLENI SANA.. HII NI MITIHANI YA DUNIA TU

    ReplyDelete
  8. wakati umefika kwa serikali kutoa vipaombele kwa huduma za afya kwa wananchi wake hasa kwa watoto kama hawa mbona bajeti ya chai wizarani zinatengwa mamilion? vipi kuhusu kuwasaidia wagonjwa wasio na uwezo? wizara ya utawi wa jamii iko wapi?

    ReplyDelete
  9. kuna matibabu ya moyo ya bure kwa watoto chini ya miaka kumi. linki hii ya facebook kuna namba ya simu ya hiyo hospitali india. https://www.facebook.com/photo.php?fbid=333415570082923&set=a.299346750156472.69060.280106802080467&type=1&theater

    ReplyDelete
  10. Huko kwetu Zanzibar hiyo hospital ya mnazimmoja ni camp ya Gestapo unapelekwa kufa tu. Uzuri wa India wala sio kwamba matajiri sana lakini sifa yao wana madaktari waadilifu sana sana tena sana. Vile vile matajiri waliona hilo hivyo wamewekeza katika vifaa na kuwarudisha madaktari waliokimbilia nje kuja kuhudumia nchi yao. India wana madaktari wengi sana sana. Wahudumu vile vile sio waomba rushwa, ila ukiwapa hawakatai, kwa sababu mishahara midogo. Nimetoka Apollo Hydrebad jhuzi. Wale wauguzi na wahkudumu wengine hawarudi nyumbani, maana ni mbali, basi tuliingia bpale alfajiri pale reception tumekuta watu wamelala. Tulipouliza tukaambiwa hawa wanakaa mbali sasa wanaogopa usafiri wa taabu wakienda watachelewa kazini na ukichelewa kazini huna kazi. Sasa unaamua mwenyewe. Hivyo wao wameamua wanaenda nyumbani wakiwa off. Hebu fikiria hapa kwetu uadilifu huo upo. Na ukiwa wodini hiyo huduma unayoipata yaani hela yako unaona kabisa inavyokutumikia unakuwa kama mfalme, ukikohoa hao wamekuja, wala hawalali kama manesi wetu hapa ambao akilala na ukamwamsha na kelele zako ama atakutukana na/au kukupiga makofi na ole wake useme. Hivyo hata wakiboresha vipi itachukua muda watu wa hapa kubadilika. Hapa Agakhan ukitaka huduma ya nesi fulltime umajiri akiwa off na umlipe pesa nzuri tu. Hiyo nimeiona vilevile.

    ReplyDelete
  11. Kidogo kidogo hujaza kibaba. Namba ya akaunti au anwani itasaidia ili tupeleke tunachoweza. Asante.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...