KAMPUNI ya Msama Promotions inatarajia kufanya uzinduzi mkubwa wa albamu ya sita ya Haleluya, ambayo inawahusisha wanamuziki wa Injili wa nchi za Afrika Mashariki.
Uzinduzi wa albamu hiyo unatarajiwa kufanyika Septemba mosi mwaka huu, ambapo kutakuwa na wanamuziki mbalimbali wa muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya nchi ambao watausindikiza uzinduzi huo.
Akizungumza mapema leo jijini Dar, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amebainisha kuwa maandalizi ya albamu hiyo yanakwenda vizuri na wanauhakika wa kufanya mambo mazuri zaidi. “Tumeshaanza maandalizi ya Haleluya Collections, tumejipanga kutoa albamu bora iliyoshiba, itakuwa ni albamu kali ya muziki wa Injili nchini na Afrika kwa ujumla,”alisema Msama.
Alieleza kuwa uzinduzi huo utafanyika pia kwenye mikoa zaidi ya saba, ambapo utaratibu wa kuteua mikioa hiyo bado unaendelea. Alisema uzinduzi huo utakuwa ni wa CD na DVD na albamu hiyo itakuwa imebeba nyimbo zaidi ya tano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...