Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – SACP. Mohammed R. Mpinga (kushoto) na Mr. Salum Yusuph - Naibu Kamishna wa Kodi za ndani TRA (kulia) wakisikiliza maswali mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari (pichani hawapo) kuhusu mwisho wa kubadili leseni za zamani za udereva utakao kuwa mwisho wa mwezi huu 30/04/2013.
Mr. Salum Yusuph - Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani TRA (kulia), akijibu moja ya swali lililoulizwa na waandishi wa habari katika mkutano ulifanyika Katika ukumbi wa mikutano wa TRA Makao Makuu Tarehe 10/04/2013.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. aya ya mwisho inaeleza kwamba lengo si kumkomoa mtu, kama hilo linazingatiwa basi kifungu namba 7B kirekebishwe, iwe ni dereva tu ndie atakaeshitakiwa, wajibu wa ku-renew leseni ni wa mwenye leseni na si wa mtu mwingine yeyote/mmiliki wa gari. mfano dereva ametumwa na gari akafanye kazi ya kubeba mizigo kwa miezi mitano mfululizo ndani ya mwanza na mmiliki anaishi dar, alipoondoka dar leseni ilikuwa hai bali imekwisha muda miezi minne baada ya kufika mwanza, mmiliki wa gari atajuaje? au mnamaana dereva akiajiliwa basi leseni yake akabidhi kwa mmiliki wa gari ili mmiliki aweze kuifuatilia kama imekwisha muda au la? hivi mnataka kila asubuhi mmiliki wa gari awe anafanya kazi ya kukagua leseni ya dereva? na kama amelazwa hospitali anaumwa na kazi zinaendelea, atoke akakague leseni ya dereva? sheria hiyo ya kijinga rekebisha haraka!!

    ReplyDelete
  2. walioko nje wa nchi wafanyeje?

    ReplyDelete
  3. Je na sisi tulioko nje ya nchi?? Serikali imelifikiria hili swala kwa makini? Lazima kuwe na exceptions.

    ReplyDelete
  4. NASHINDWA KUELEWA VIONGOZI WA TANZANIA WANAPO TOKA NJE YA NCHI KWA NINI HAWAJIFUNZI MAZURI YALIOKO HUKOOOO???? KWA SWALA LA LISENI KWANINI WAMLAZIMISHE MTU KUBADILI LISENI AMBAYO AMESHAA ILIPIA KWA MUDA MAALUM NA ITAFIKA SIKU ITAMALIZA MDA WAKE NA HAPO MHUSIKA AFUATE TARATIBU ZA KUPATA LISENI MPYA. BILA KULAZIMISHANA KWANI INASEMEKANA NI NJIA YA UKUSANYAJI MAPATO KWA NGUVU LAKINI TUNAKUMBUKE HII NCHI NI YETU SOTE LEO UKO WEWE NA KESHO ATAKUWEPO MWINGINE TUHURUMIANE WATANZANIA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...