-Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na uongozi wa Kampuni ya Utafiti na Uzalishaji mbegu bora za mazao ya mboga ya RIJK ZWAAN jana katika kitongoji cha De Lier nje kidogo ya jiji la The Hague.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa pamoja na Malkia Beatrix wa Uholanzi wakati walipomtembelea Malkia huyo katika makazi yake Rasmi jijini The Hague jana.Rais Kikwete yupo nchi Uholanzi kwa Ziara rasmi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Frans Timmermans akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo jijijini The Hague na kufanya naye mazungumzo rasmi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo Rasmi na ujumbe wa Serikali ya Uholanzi ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya nchi za nje wan chi hiyo Bwana Frans Timmermans jijini The Hague Uholanzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...