MRAJIS wa Baraza la Sanaa Zanzibar (BASAZA), Khadija Batash akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada kutolewa kwa taarifa za kifo cha Msanii mkongwe Nchini, Fatma Bint Baraka ‘Bi Kidude’ nyumbani kwa msanii huyo Rahaleo mjini Zanzibar.
MTENDAJI wa Busara Promotions, Stela Steven akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada kutolewa kwa taarifa za kifo cha Msanii mkongwe Nchini, Fatma Bint Baraka ‘Bi Kidude’ nyumbani kwa msanii huyo Rahaleo mjini Zanzibar.
WAANDISHI wa Habari kutoka vyombo mbali mbali wakiwa kazini katika makaazi ya Msanii Bi Kidude muda mfupi baada ya kufariki kwa msanii huyo.
WATENDAJI wa Busara Promotins wakijadiliana jambo nje ya nyumba ya msanii Bi Kidude muda mfupi baada ya kufariki.
MJUKUU wa marehemu Bi Kidude, Bwana Baraka, akitoa taarifa za mazishi kwa waandishi wa habari nyumbani kwa marehemu Rahaleo mjini Zanzibar.
WAFIWA wakiwa nyumbani kwa marehemu.
MKURUGENZI wa Kikundi cha Taarab cha TAUSI, Mariam Hamdani akizungumza na Waandishi wa Habari nyumbani kwa marehemu Bi Kidude.
Sihaba Ismail mmoja wa watu waliofundishwa kazi za kufunda wari na dawa asilia na Bi Kidude akielezea anavyomfahamu marehemu.
MSANII wa Taarabu asilia, Makame Faki akielezea jinsi Bi Kidude alivyokua akiimudu sanaaa ya taarabu na unyago.
Picha zote na Haroub Hussein wa Globu ya Jamii, Unguja
No one cared for her including SMZ, now see the outpouring of grief. Watanzania sisi ni wanafiki big time!!
ReplyDeleteSijawahisikia serikali ama taasisi binafsi kufanya harambee ya matibabu kwa wasanii wa kitaifa kama huyu Bi kidude na zaidi zanzibar wapo wenye mfano kama yeye walikufa hivhiv wanajiona. Wengi waliugua na kufa bila serikali kushituka. Sasa tunabakia kumsifia mfuu.Ameacha mambo mazuri duniani katika tasnia ya sanaa.
ReplyDeletelakini, ni vipi alijiandaa kwa makaazi ya milele huko kwake M/Mungu. Hakika M/mungu ndie ajuae ni nyumba ipi ya kumuweka
RIP mtani wangu Bi K mungu akusamehe makosa yako kwani hakuna bin Adam mkamilifu.