Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam hatua ya sita bora imeendelea leo kwa michezo mitatu, ambapo kwenye Uwanja wa Kinesi, Abajalo imeifunga Friends Rangers bao 1-0. 
Bao hilo limefungwa na Waziri Omary katika dakika ya 35. Abajalo sasa wamefikisha pointi 7 wakishika nafasi ya pili. Kwenye Uwanja wa Makurumla, Boom FC imetoka sare ya bao 1-1 na Read Coast. 
Bao la Red Coast limefungwa na Idrisa Pandu katika dakika ya 28 wakati lile la Boom limefungwa na Janka Ally katika dakika ya 41.Red Coast wanaendelea kuongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 8.
 Kwenye Uwanja wa Airwing, Sharif Stars imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Day Braek. Bao hilo limefungwa na Dovan Kanyinda katika dakika ya 89 na hivyo kufikisha pointi 6 katika michezo minne iliyocheza. 
 Kila timu hadi sasa imecheza michezo minne na ligi hiyo itafikia tamati Aprili 27 ili kupata timu tatu za juu zitakazocheza hatua ya Kanda. 

 Imetolewa na Mohamed Mharizo
 Ofisa Habari wa Chama cha Mpira wa Miguu 
Mkoa wa Dar es Salaan (DRFA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...