
Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu
Katibu Mkuu wa CHADEMA Mhe. Zitto Kabwe
--
Nimekuwa naulizwa kuhusu Habari za mama yangu Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola. Nawajibu watu Kwa ujumla kwamba
“Moja, mie sio msemaji wa familia. Ni basi tu katika watoto wa mama yetu mie najulikana zaidi na hivyo mama anaitwa Mama Zitto. Kwetu Kigoma haitwi hivyo, ama Ni mama Salum au mama Lulu.
Pili, hili Ni suala la polisi. Lipo polisi na linashughulikiwa na polisi. Nisingependa kulisemea wakati Ni suala linalochunguzwa na polisi. Mama yangu Ni mama wa kawaida wa kitanzania kama mama mwingine yeyote yule. Matukio ya namna hii yamezagaa nchi nzima. Hivyo suala lake litashughulikiwa kama yanavyoshughulikiwa masuala mengine yote ya Watanzania. Polisi wakimaliza uchunguzi wao naamini hatua mwafaka zitachukuliwa.
Ushauri- tuwe makini na “Agente provocatuers” au in English “provocation agents” nyakati kama hizi. Calmness is the best protection against provocations. Nadhani mmenipata”
Nawatakia Kila la kheri katika kazi za ujenzi wa Taifa letu na kuimarisha Umoja na mshikamano wa Watanzania dhidi ya ufisadi, umasikini na ugandamizaji.
Majibu haya ameandika kupitia mtandao wa Kijamii wa facebook.
Zitto umeelezea vzr sana kaka,
ReplyDeleteIf you have nothing to say, why do you say something at all? Silent is gold bro, not for politicians of course. Pole sana na swala la mama, kama lipo....
ReplyDeleteZito kweli wewe ni Zito...nimependa sana majibu yako your so smart I like it..
ReplyDeleteSijaona umejibu nini. Mimi binafsi nilistushwa na habari hizi na kuwa na maswali lukuki. Mhe. Zito maelezo yako hayajanijibu hata robo swali. Kama ulitaka police ndio watoe taarifa rasmi wewe maelezo haya shallow ni ya nini? Any ways its Ok. Pole sana kaka
ReplyDeletekaka njoo cuf watakuuwa huko hawakutaki we jitie kinganganizi tu
ReplyDeletePole sana Zito, na wewe unayesema angekaa kimya una chuki binafsi.
ReplyDeleteNami namshangaa! pole sana kwa hili la mama lakini.
ReplyDeleteSio kila mtu ana uwezo wa kuelewa alichosema zito.
ReplyDelete