Na Mwandishi
Maalum
Tanzania
imeungana na mataifa mengine
katika kuendelea kukemea vitendo vya
udhalilishaji wa kimapenzi vinavyoendelea kufanyika dhidi ya wanawake,
watoto na hata wanaume katika maeneo yenye migogoro.
Kwa siku nzima
ya jumatano, Baraza Kuu la
Usalama, lilikuwa na mjadala kuhusu wanawake, amani na usalama, ambapo wazungumzaji zaidi ya 60 waliozungumza, licha
ya kukiri kwamba kumekuwa na mafanikio
fulani katika kukabiliana na unyanyasaji na udhalilishaji huo lakini
hali bado ni ngumu na jitihada zaidi zilikuwa zinahitajika.
Majadiliano hayo
ambayo yamefanyika chini ya urais
wa Rwanda ambaye ndiye anayeongoza Baraza hilo kwa mwezi huu wa April,
yalifunguliwa na Katibu Mkuu Ban Ki Moon
kwa kuwasilisha Taarifa yake
iliyotoa tathimini ya kina kuhusu hali ya wanawake, amani na usalama katika
maeneo mbalimbali ambako migogoro bado inaendelea.
Ujumbe wa
Tanzania katika mkutano huo uliongozwa na Dr. Justin Seruhere, Afisa Ubalozi
Mwandamizi. Ambaye akizungumza kwa
akizungumza niaba ya serikali,
alisema pamoja na kuunga mkono hoja ya kufikishwa mbele ya sheria watuhumiwa wa
uharamia huo, na kuongeza kasi ya kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo, Tanzania pia inasisitiza
matumizi ya vyombo vya kisheria
vya ndani ya nchi husika katika
kuwashughulikia watuhumiwa .
Akasema kutokana na ukubwa wa tatizo na uyeti wake, na
hasa ikizingatiwa pia kwamba watuhumiwa
hao wanatakiwa kushtakiwa na kuhukumiwa
na vyombo madhubuti, ni vema basi vyombo
hivyo vikajengewa uwezo wa kutekeleza jukumu hilo.
Hata hivyo akasema ikidhihirika
kwamba nchi husika haina
vyombo imara kuifanya kazi hiyo, na kama ambavyo mara nyingi imeshadhihirika hivyo. Basi Tanzania inashauri nchi husika ziwe tayari kuwahamishia watuhumiwa hao katika
vyombo vya sheria vya kimtaifa kama
vile Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC).
Akaueleza mkutano huo kwamba vyombo hivyo vya
kimataifa licha ya kasoro mbalimbali zina raslimali na uwezo mkubwa
wa kuwashughulikiwa wahalifu.
Akasema Tanzania
inahimiza na kuunga mkono hoja ya
kuiongezea uwezo ICC ili iweze
kutekeleza majukumu yake na hasa ikizingatiwa kwamba kwa sasa ndicho chombo
kilichopo na kinachotegemewa na jumuiya ya kimataifa.
Aidha Tanzania
katika mchango wake imesisitiza haja na umuhimu wa kuwawezesha
wanawawake na watoto wa kike ili waweze kushiriki katika masuala ya ulinzi na usalama na vilevile
katika utoaji wa maamuzi yanayohusu uzuiaji wa migogoro na utatuzi wake.
Akaongeza kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajivunia hatua yake ya
kuongeza askari wanawake katika shughuli za ulinzi wa amani zinazosimamiwa na
Umoja wa Mataifa ambapo kuna askari
wanaweke 200 hadi sasa . Na kwamba Tanzania imejipanga kuongeza idadi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...