Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota akionyesha simu mpya na ya kisasa (smart phone) zinazopatikana katika vituo vyote vya huduma kwa wateje nchini kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya BANDO NA TTCL pamoja kampeni ya BASTI iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.kulia ni mkuu wa Mauzo Bw. Kisamba Tambwe.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa maendeleo ya bidhaa wa TTCL Ernest Isaya, afisa mkuu wa mauzo na masoko Peter Ngota na Mkurugenzi wa Mauzo Bw. Kisamba Tambwe.
Afisa mkuu wa mauzo na masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota akionesha bango lenye punguzo kubwa la bei ya Intanet wakati wa uzinduzi wa kampeni ya BASTI uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Mauzo wa TTCL, Kisamba Tambwe. 

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Bando mpya mmeleta modem? Manake kwa muda sasa wengine tumesubiri modem zenu weee but where!!!! Jumped ship to other providers - Smile please and take a bow!

    ReplyDelete
  2. hongera sana ttcl,for real u need to strengthen ua turnover strategy otherwise competition will lock you out,..KING JOJO

    ReplyDelete
  3. TTCL HATA IKKIFA HAO UNAOWAONA HAWANA CHOCHOTE CHA MAANA.NI VIGUMU UKIFANYA KAZI KAMA ROBOTI DUNIA YA LEO WAKATI DUNIA INABADILIKA WEWE HUTAKI KUBADILIKA.

    TTCL WAFANYAKAZI HAWAKO CREATIVE NA HII NAFIKIRI INACHANGIWA NA KUAJIRI KWA KUJUANA NA KUKOSA MFUMO WA KUWAJIBISHANA.

    NILISHAPELEKA SIMU YA WIRELESS KUFANYIWA MATENGENEZO IKAKAA MWAKA NA MIEZI MITATU MOROGORO OFFICE.KUJA KUIPATA IKAONEKANA KUNA MFANYAKAZI ALIPELEKWA KWAKE AKAWA ANATUMIA NA FAMILIA YAKE.

    NILILILAMIKA SANA,ILA WALIKUWA WANANIONA KAMA HAYAWANI.

    KUPOTEZA MTEJA MMOJA DUNIA YA LEO,NI KAZI KUMRUDISHA.

    BADIRIKENI NA DUNIA IMEBADILIKA.ACHENI KUFUATA WANASIASA,TUMIENI TAARULAM ZENU NA IKIBIDI MFUKUZANE KAZI WAAAJIRIWE WATU WENYE UCHUNGU NA SI MISHAHARA.

    ReplyDelete
  4. TTCL kipindi kile cha mobile phone zao walikuwa juu sana lakini walijishusha wenyewe kwani hawapo creative,wamekaa kizembe zembe,waliajiriwa vijana ambao walikuja kuambukizwa na wazee uzembe nao mpk sasa wamekuwa wazembe zaidi.Soko la kampuni za simu lina ushindani sana wenzao sasa wanatanganza bei za kupga mtandao mmoja kwenda mwingine na wao ndiyo wameamka kuuza byndle ambazo wenzao walishapunguza kitambo.Isitoshe hizo bei zao bado zipo juu.Wao sababu wamelala ilitakiwa bundle wauze kwa bei ya chini zaidi ili wavute wateja upya.Kingine ni kuwa inaonekana hawa jamaa hawana bajeti ya kuwezesha marketing team yao iwe strong sababu serikali ina mkono wake na pesa ya serikali haitoki kama ya private.Hawa jamaa naamini wakibadili na kuiwezesha marketing team yao na kuipa bajeti nzuri wanaweza kurudi kwenye gemu sbb biashara ya sasa ya telecom ni matangazo kama hauna bajeti ya marketing iliyoshiba umeliwa.Kitu kingine cha ajabu ni kwamba wafanyakazi wao pia hawana hizo line za TTCL,je wanawezaje kushawishi wengine wanunue?Nadhani pia hata modern systems hawana za kuleta ushindani na wengine.WAMEFUFUKA JUZI KWENYE MAKUBALIANO YA TARIFF TOKA MTANDAO MMOJA KWENDA MWINGINE,ila walikuwa wamelala usingizi wa pono.Natumai database ya TTCL ya wateja kwa sasa imebaki na active wateja wa landline tu na si mobile phone.Pia waachane na modem zilizo kama gobole,dunia imebadilika watafute modem ndogo sana walete kwenye market,huwezi kunibebesha mzigo mkubwa wa li-moderm kila mtu anajua umebeba moderm.

    ReplyDelete
  5. hawa bado sana. Mi nimeenda ofisini kwao pale Samora sikuona faida ya kwenda hapo. Hawatauza hizo huduma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...