Mkurugenzi wa Idara ya Utalii , Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Bw. Ibrahim Mussa (kushoto) akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Wizara ya Utalii ya China Bw. Zhu Shanzhong juu ya masuala mbalimbali ya uhusiano baina ya nchi hizi mbili hususan katika sekta ya utalii wa Tanzania katika soko la China.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Dk. Aloyce Nzuki (kulia) na Mkurugenzi Msaidizi wa Malikale John Kimaro wakifuatilia mazungumzo hayo kwa umakini.
Balozi wa Tanzania nchini China Philip Marmo (kulia) na Mbunge wa Ngorongoro Mhe. Kaika Telele wakifuatilia mazungumzo baina ya serikali ya Tanzania na China kuhusiana na sekta ya utalii nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (kushoto) na Kaimu Mhifadhi wa Mamlaka ya Ngorongoro Bruno Kawasange wakifuatilia mazungumzo hayo.
Viongozi wa Serikali ya China wakifuatilia majadiliano.
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Ibrahimu Mussa (kushoto) akipokea zawadi maalum ya stempu mbalimbali za China kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Wizara ya Utalii nchini China Zhu Shanzhong mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao.
Mkurugenzi wa Utalii Ibrahimu Mussa na Balozi Philip Marmo wakiwa na Makamu Mwenyekiti wa Wizara ya Utalii ya China Bw. Zhu Shanzhong.Picha zote na mdau Pascal Shelutete, TANAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Welcome to Tanzania the land of Kilimanjaro,Zanzibar,the Serengeti and the business bridge to great lakes countries via Dar es Salaam Port.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...