Picha ya mchoro ya kivuko cha  Dar es Salaam – Bagamoyo kitakavyokuwa.
 Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Marceline Magesa (mwanamke) , na mwakilishi wa kampuni ya  JOHS GRAM HANSSEN A/S ya  Denmark  Andreas Gottrup wakiweka  saini mkataba wa ujenzi wa Kivuko  cha Dar es Salaam- Bagamoyo leo jijini Dar es Salaam, katika hafla iliyoshuhudiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (aliesimama katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadick(alie vaa  shati la kitenge) Balozi wa Denmark nchini Tanzania  Mh, Johnny Flinto (mzungu aliesimama  mstari wa nyuma). Pamoja na watendaji wakuu wa  Wizara ya Ujenzi. 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sadick Mecky (kulia) akizungumza wakati wa  hafla ya uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa  Kivuko cha Dar es salaam – Bagamoyo. Kivuko hicho kitagharimu shilingi 7.91 bilioni za kitanzania. Mwengine ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli. 
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kulia) akiongea na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mh. Johnny Flinto,katika  sherehe ya uwekaji  saini mkataba wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaa- Bagamoyo (April 25, 2013).
 baadhi ya viongozi wakiwa katika meza kuu
Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya TEMESA, Prof. Idrisa Mshoro (kulia) akimueleza  jambo  Mwakilishi wa  kampuni ya JOHS GRAM HANSSEN A/S ya Danmark , Andreas Gottrup wakati wa sherehe za uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaam- Bagamoyo jijini Dar es  Salaam(April,25,2013). 
 baadhi ya wadau wa wizara ya ujenzi wakishuhudia tukio hilo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Marceline Magesa (kulia) akizungumza  katika hafla ya uwekaji saini  mkataba wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaam- Bagamoyo leo jijini . Kivuko hicho  kitakuwa na uwezo wa  kubeba watu 300 , kitagharimu  shilingi7.91 bilioni.(bilioni7.91 za tz).Pichani  kutoka kulia ni Waziri wa Uchukuzi Dkt,John Magufuli,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Mecky Sadick, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi , Balozi Herbert Mrango.Picha zote na Mwanakombo Jumaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mi-stew mimi nakuheshimu, lakini uncle usiajiri waandishi wa habari mlegezo, tangu lini eti una m-refer mtu kwa jinsia(sex discrimination) au kwa rangi ya ngozi yake, haipendezi, muandishi angeandika "aliyevaa suti ya kahawia" na wa nyuma mwenye shati jeusi and KIPARA ng`oto.

    ReplyDelete
  2. Hivi kweli kwenda Bagamoyo watu wanahitaji kivuko?

    ReplyDelete
  3. Saini KAIWEKWI bali usahihi ni KUTIWA saini.Najua kwa wale wenye matatizo ya matusi syndromes watatafsir kutokana na matatizo yao lakini hicho ndich kiswahili sanifu.

    ReplyDelete
  4. mmechungua hii boti inahali gani? isije ikawa kama zile zilizowauwa watu zanzibar au bara haziwauwi zina uhakika?

    ReplyDelete
  5. Hahahahaha

    Mtoa Maoni wa kwanza umenichekesha saaana umeifanya siku yangu kuwa nzuri na stress zimeshuka!

    Heee na wewe kusema Kipara Ng'oto (mwenye Kipara) ambaye ni mwenye (shati la Kitenge), sasa hapo utakuwa umetunanga wengi maana wengi tumezeeka na tuna Vipara vya uhalaza vichwani na hiyo sio age Descrimination?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...