Picha ya
mchoro ya kivuko cha Dar es Salaam –
Bagamoyo kitakavyokuwa.
Mtendaji Mkuu wa
TEMESA Mhandisi Marceline Magesa (mwanamke) , na mwakilishi wa kampuni ya JOHS GRAM HANSSEN A/S ya Denmark
Andreas Gottrup wakiweka saini
mkataba wa ujenzi wa Kivuko cha Dar es
Salaam- Bagamoyo leo jijini Dar es Salaam, katika hafla iliyoshuhudiwa na
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (aliesimama katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam Mecky Sadick(alie vaa shati la
kitenge) Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mh, Johnny Flinto (mzungu aliesimama mstari wa nyuma). Pamoja na watendaji wakuu wa Wizara ya Ujenzi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam Sadick Mecky (kulia) akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji saini mkataba wa ujenzi
wa Kivuko cha Dar es salaam – Bagamoyo.
Kivuko hicho kitagharimu shilingi 7.91 bilioni za kitanzania. Mwengine ni Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli.
Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Magufuli (kulia) akiongea na Balozi wa Denmark nchini Tanzania
Mh. Johnny Flinto,katika sherehe ya
uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa
kivuko cha Dar es Salaa- Bagamoyo (April 25, 2013).
baadhi ya viongozi wakiwa katika meza kuu
Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya TEMESA, Prof. Idrisa Mshoro (kulia) akimueleza jambo Mwakilishi wa kampuni ya JOHS GRAM HANSSEN A/S ya Danmark , Andreas Gottrup wakati wa sherehe za uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaam- Bagamoyo jijini Dar es Salaam(April,25,2013).
baadhi ya wadau wa wizara ya ujenzi wakishuhudia tukio hilo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Marceline Magesa (kulia) akizungumza katika hafla ya uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaam- Bagamoyo leo jijini . Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba watu 300 , kitagharimu shilingi7.91 bilioni.(bilioni7.91 za tz).Pichani kutoka kulia ni Waziri wa Uchukuzi Dkt,John Magufuli,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadick, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi , Balozi Herbert Mrango.Picha
zote na Mwanakombo Jumaa.
Mi-stew mimi nakuheshimu, lakini uncle usiajiri waandishi wa habari mlegezo, tangu lini eti una m-refer mtu kwa jinsia(sex discrimination) au kwa rangi ya ngozi yake, haipendezi, muandishi angeandika "aliyevaa suti ya kahawia" na wa nyuma mwenye shati jeusi and KIPARA ng`oto.
ReplyDeleteHivi kweli kwenda Bagamoyo watu wanahitaji kivuko?
ReplyDeleteSaini KAIWEKWI bali usahihi ni KUTIWA saini.Najua kwa wale wenye matatizo ya matusi syndromes watatafsir kutokana na matatizo yao lakini hicho ndich kiswahili sanifu.
ReplyDeletemmechungua hii boti inahali gani? isije ikawa kama zile zilizowauwa watu zanzibar au bara haziwauwi zina uhakika?
ReplyDeleteHahahahaha
ReplyDeleteMtoa Maoni wa kwanza umenichekesha saaana umeifanya siku yangu kuwa nzuri na stress zimeshuka!
Heee na wewe kusema Kipara Ng'oto (mwenye Kipara) ambaye ni mwenye (shati la Kitenge), sasa hapo utakuwa umetunanga wengi maana wengi tumezeeka na tuna Vipara vya uhalaza vichwani na hiyo sio age Descrimination?