NAIBU Waziri wa Miundo Mbinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Issa Haji Usi na Jaji Mstaafu Jaji John Mkwawa wataongoza kamati ya ujenzi wa jengo la Yanga lililopo mtaa wa Mafia.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Ridhiwan Kikwete ambaye ametangaza leo orodha ya wajumbe tisa atakaosaidiana nao katika kuhakikisha wanajenga jengo hilo lililopo mtaa wa Mafia na Nyamwezi.
Kikwete alisema kuwa Naibu Waziri huyo wa Zanzibar ndio atakayekuwa Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo akisaidiana na Jaji John Mkwawa.
Alisema wajumbe wengine ni Baraka Ingangula ambaye ni mtaalamu wa majengo na kwamba atasaidia kuwapa mchoro wa kujenga jengo la kisasa lenye hadhi na imara.
"Inabidi tutafute mtu ambaye atatusaidia katika usanifu wa jengo tukalojenga hatuwezi kujijengea tu siku mbili limeanguka kama mengine yanavyoanguka na kutuletea shida."alisema Kikwete.
Mbali na Igangula pia amemteua Allan Magoma kutoka Tanzania Investment Bank, Charles Palapala (mfanyakazi wa benki), Izack Chanje (Injinia) na wakili Mavalle Msemo.
Kikwete alisema kuwa mbali na wajumbe hao pia ameunda kamati ndogo ambayo itakuwa na jukumu la kufatilia masuala mbali mbali ya ujenzi wa jengo hilo ambayo itaongozwa na Katibu wa Yanga Laurance Mwalusako akisaidiwa na Beda Tindwa na Mohamed Milando.
Kikwete alisema kuwa wiki ijayo anatarajia kukutana na kamati yake na kupeana majukumu ikiwa ni pamoja na kupokea michoro mbali mbali ya majengo ambayo wataiangalia na kujua thamani alisi ya jengo ambalo watalijenga.
“Tumeshawapa notisi wapangaji wa jengo hilo ili watupishe tuanze ukarabati haraka iwezekanavyo. Tunataka tuwe na jengo la kisasa ambalo litakuwa na manufaa kwa klabu kwa kuhakikisha linakuza uchumi wa timu.
“Naahidi kujenga ghorofa kubwa lenye hadhi, ndio maana nimeteua wajumbe wenye uelewa mkubwa nitakaosaidiana nao,” alisema Ridhiwani.
Kila la heri
ReplyDeleteover ambitious!!
ReplyDelete