Wanawake na wasichana wa Dar es salaam na mikoa ya jirani Kitchen party gala ipo on tayari.

Mwaka jana ile ya mwisho ya mwezi wa kumi tulifanyia Diamond jubelee VIP hall na ukumbi ulishona sana sana.Kulikuwa na mapungufu kadhaa ambayo sitapenda yajirudie
 this time.Najua ni mara chache shughuli kukosa upungufu fulani lakini kulirudia kosa ndio kosa zaidi.

Sasa mwaka huu tumepata ukumbi mpya kabisa upo ndani ya jengo la GOLDEN JUBELEE.Hili jengo ni jipya lipo pembeni ya jengo la PPF Tower mjini kabisaaa.

Ukumbi huo unaingiza watu 1000 tu na ndio idadi tunayoitaka siku hiyo.
Service zao ni za kihoteli kabisa na wao ndio wataserve kila kitu.Ukumbi huu uko chini ya JB Belmonte hotel hivyo wao ndio watatoa huduma za chakula.Chakula chetu kitakuwa kwenye hadhi ya starter,main course na desert.
Hivyo tumeona tuadvance ili kukidhi mahitaji yako ya kihuduma,mazungumzo yetu ya siku hiyo na burudani.

Na kwasababu tumeadvance kihuduma na shughuli kwa ujumla  kiingilio chetu this time kitapanda kitakuwa Tsh 40,000/= Ukumbi una vyoo vingi vipya na visafi na wa hadhi ya kimataifa.Pia najua kina mama ndio waandaaji wa shughuli mbalimbali za kifamilia,marafiki,ukoo mje muone ukumbi huu mpya.Hawa wana kumbi 4 katika jengo hili hili.Unaoingiza watu 1000,600,400 na 150 mkuje muone maana tunapata taabu sana ya kumbi  hasa kama unataka maeneo ya town.
Tutakuwa na wasemaji wa ndani na nje ya Tanzania.
DRESS CODE:Tusisahau dress code yetu ya siku hiyo imekuwa inspired na bendera ya nchi yetuTanzania.

TAREHE:Kparty gala itakuwa jumamosi ya tarehe 27 april 2013.Kuanzia saa tano asubuhi mpaka kumi na mbili jioni.
 Kwa lolote piga namba hii 0787583132 na 0657442255.

ASANTENI

Ognaniser
Dina Marios
!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. nimefurahi sana kujua kwamba rangi za bendera ya tanzania itatumika natamani ningekuwepo.hivi ndio vitu tunataka kusikia.

    ReplyDelete
  2. This suound more like kutangaza ukumbi kuliko Party yenyewe. Badoo sana - kwa mimi msomaji wa mara ya kwanza shughuli hii inahusu nini? inawalenga akina nani? Wasemaji wa nje ni wanasema nini? na wandani je? Maswali kede kede.

    ReplyDelete
  3. vyoo vyenye hadhi ya kimataifa??ha ha ha ha dada yangu dina unanifurahisha sana...kwani kuna vyoo vyenye hadhi ya kitaifa?hebu nifafanulie vikoje plz..nawatakia kila la kheri kwenye hiyo event.

    mdau
    uswis

    ReplyDelete
  4. Angalieni tu hilo jengo lisije wadondokea mkiwa kwenye kula kunywa yenu.. kafanyeni hiyo shughuli kwenye uwanja wa wazi, jangwani poa., mmeonywa tayari..75% ya majengo marefu hapo mjini hayafai kwa matumizi ya binadamu

    ReplyDelete
  5. Hongereni kwa kuchagua mavazi yawe rangi ya kitaifa, unaonaje pia ungekuza kiswahili maana maneno yaliyochnaganywa(kiswaenglish) yanatafsirika kiswahili bila taabu

    ReplyDelete
  6. I AGREE WITH YOU ANNON 03.10.00AM ITS NOT SAFE FOR NOW I ALSO SUGGEST OPEN SPACE KARIMJEE, LEADERS, POSTA CLUB, JANGWANI ETC

    ReplyDelete
  7. HIVI KITCHEN PARTY HII NI YA KUHUSU NN LABDA INGEELEZWA HAPA TUKAJUA SISI AMBAO HATUJAWAHI KUJA NA TUNGEPENDA KUJA. KAMA NI MAMBO YA KUWAHUDUMIA WANAUME, SAMAHANI IMEPITWA NA WKT MANA HAO WANAUME TUNAWAKUZA SANA NA WALA HAIWABADILISHI TABIA. PIA TUNGEPENDA HAO WANAUME NAO WAJIFUNZE JINSI YA KUTUHUDUMIA, MANA MAHUSIANO NI BOTH SIDES. UTUMWA MAMBO LEO KWA WANAWAKE, SORRY

    ReplyDelete
  8. Ni kitu kizuri Dina hasa kwa sisi tulowahi kuhudhuria na kupata mapya mengi,labda kwa wageni ungefafanua vitu muhimu kwao ili waelewe nini hasa kinafanyika, mfano wawezeshaji mada, mada zitakazozungumziwa.
    Kiukweli mwenye nafasi yake hii si kitu ya kukosa kwani kila aliyehudhuria zilizopita alipata la kujifunza jipya ama kukumbusha ya msingi ikiwemo kiuchumi, kijamii hata kimapenzi pia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...