Michuzi,
Tukiwa katika maswala ya ujenzi usiofuata viwango na masharti ya ujenzi, nilikumbana na hoteli iliyoko Shinyanga mjini ambayo imemalizika na wateja wanaishi. Cha kushangaza ni kuwa ngaziimechomoza katika kila corridor ya hoteli hii. Pia ngazi hizo hazilingani. Utakuta nyingine ndoogo na zingine kubwa, kiasi inatia wasiwasi kuhusu usalama wa watumiaji wa hili jengo. Mathalan ikitokea dharura ama hatari yoyote kaam vile moto na majanga mengine matokeo yanajulikana kwa kuangalia design failure hii.

Halimashauri ya Shinyanga mjini mpooo?
Ni mimi mdau SHY TOWN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Madau wa SHY umeshawai kujenga nyumba?

    If not please nyamaza

    ReplyDelete
  2. Hao ndiyo ma-engineer wetu mkuu. Kazi kujiita Engineer Fulani wakati kazi wanachemsha. Angalia hiyo design, sijaona kitu kama hiki duniani.

    ReplyDelete
  3. Hapo kwenye dharura tupo pamoja, ila kulingana kwa ngazi, ngazi zenyewe haziendi kokote. Nadhani ni mapambo tu, hakuna haja ya kulingana wala kufuata viwango vya TBS.

    ReplyDelete
  4. Hapo tunazungumzia swala la SAFETY hizo ngazi hazitakiwi kuweko, hawa engineer na arcthitecter wa bongo ni noooooma sijui wamekwenda shule za wapi

    ReplyDelete
  5. Tatizo sio wahandisi na wasanifu majengo, tatizo ni watu kutafuta unafuu ulipitiliza wa kutumia watu wasio wataalamu wa ujenzi, wangapi mnajenga nyumba zenu mkitumia wahandisi na wasanifu majengo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...