Hilo linaloonekana pichani ni furushi la chuma (steel roll), lililodondoka toka kwenye semitrailer iliyokuwa inatoka bandarini kuelekea viwandani pale Buguruni,jijini Dar es Salaam katika makutano ya barabara ya Uhuru na Mandela Road.

Sijui ingekuwaje kama lingemdondokea mpita njia au hata gari nyingine,maana hapo tu ni muda wowote linaweza sababisha hadha ya foleni! Mwenyezi Mungu amenusuru hiyo, tumshukuru sana kwa kweli.

Mdau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Nimepita hapo saa kumi na mbili wakati naenda job mashuhuda wanasema mwendesha Bodaboda alfajili amepita kwa kasi na kuligonga kwa kuwa kulikuwa na kiza hakuliona amekufa hapohapo

    ReplyDelete
  2. Lingine nusura lianguke toka kwenye semitrailer pale ubungo stand ya mkoa leo 19/4/2013

    ReplyDelete
  3. Jamani hiii ni balaa gani?? Aliyedondosha kwanini hajachukua hatua, pili polisi kazi yao nao ni kushangaa tu au inabidi kuchukua hatua immediate. Wananchi hata hawajui waripoti wapi mambo kama hayo yanapojitokeza kwa kuwa umma hauelezwi masuala hayo. tayari mmoja amepoteza maisha kwa uzembe wa mwingine, jamani hivi ni kweli ndiyo inavyotakiwa iwe watz!

    ReplyDelete
  4. Jamani mjifunze kazi za kusafirisha mizigo kiusalama. Kuna strap zinazotumika ambazo hata hutumii nguvu kufunga mzigo wako. Mlete watu huku Ughaibuni mjifunze uchukuzi wa bidhaa kwenye malori. Mfanye mambo kama yanavyofanywa duniani!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...