Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akimsikiliza Kaimu Mkuu wa hifadhi ya Mikumi,Bwa.Datomax Selanyika wakati alipokuwa akimuelezea faida za kuhifadhi Mbuga za Wanyama na kutunza maizngira ya Mbuga hizo,aidha pia Dotomax alizungumzia mipango na mikakati ya kuihamisha barabara ya lami itokayo Dar kuelekea Tunduma ambayo imekatiza ndani ya hifadhi na alifafanua pia kuhusiana na faida ya kuihamisha barabara hiyo.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza na Wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya
Msingi Kilosa Town.Kinana alikuwemo Wilayani humo kwa ajili ya
kuimarisha chama na kukagua miradi mbalimbali ya chama hicho.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi-CCM,Nape Nnauye akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Kilosa Town,Nape aliwaasa wakazi wa Kilosa kuwa makini na mambo ambayo wamekuwa wakiambiwa kutoka kwa vyama vingine ambavyo vimekuwa vikipotosha ukweli wa mambo kuhusiana na mambo mbalimbali yanayowahusu.
Ndugu Kinana akiagana na Mbunge wa Jimbo la Kilosa,Mh.Mkulo
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akipokelewa na wanachama wa chama hicho mara baada ya kuwasili Wilayani Gairo mapema jana usiku akitokea Wilayani Kilosa sambamba na ujumbe wake wa CCM,tayari kwa kukagua miradi mbalimbali zikiwemo shughuli za maendeleo za chama hicho mapema leo.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...