Na Abdulaziz Video

Baadhi ya Abiria na Wasafishaji wa Abiria wilayani Nachingwea,mkoa wa Lindi wametishia kuandamana na kususia kutumia kituo kipya cha Mabasi wilayani huo kutokana na kutokamilishwa kwa miundo mbinu ikiwemo kutowepo kwa sehemu ya kupumzikia Abiria.Umeme,maji na Umbali wa kituo cha Mwisho hadi kituo kikuu kipya ambacho kipo pembezoni mwa mji.

Wakizungumza na mtandao huu,jana Ahmeid Mmow na Abdallah Ng’itu kwa niaba ya abiria waliitaka Halmashauri hiyo kuharakisha inakamilisha huduma walizobainishiwa na uongozi wa wasafirishaji ikiwemo uwepo wa kituo kidogo cha kushushia abiria katikati ya mji ili kupunguza gharama huku wengine wakiwa walemavu na wagonjwa ambao hawana uwezo wa kugharamia bodaboda hadi kwenye kituo hicho kipya.

Mmow alisema kuwa abiria hawana tatizo la kituo hicho kuamishwa bali wanachohitaji ni kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana na kuwa bila kufanya hivyo wasafiri wa wasafirishaji watafanya maandamano makubwa kupinaga hatua ya halmashauri hiyo kuwamisha kituo bila kukamilisha mabmbo muhimu.

“ Hatuna tatizo la kuhamia kwenye kituo hicho kipya bali tunachohitaji ni kuhakikishiwa halmashauri inakamilisha mahitaji hasa jengo la kupumzikia abiria na warejeshe vituo vingine”alisema Mmow.

Uamuzi wa Halmashauri hiyo ya Wilaya kufunga kituo cha Mabasi cha awali kimezua malalamiko makubwa kufuatia uwepo wa kituo kipya kuwa nje ya mji na kupelekea ongezeko Kubwa la gharama za usafiri na uhakika mdogo wa usalama wao pindi basi litapoingia usiku au Alfajiri kwa kuanza safari.

Mwenyekiti wa wasafirishaji wilayani Salum Jabu alisema kuwa kufuatia tatizo hilo ambalo kwa kiasi kikubwa kinawaathiri wasafiri wengi ambao wanatoka nje ya mji kwani wanakosa mahali pa kulala kwani awali abiria wengi ambao hawana uwezo wa kulala kwenye nyumba za wageni walikuwa wanapata mahali pa kulala kwenye ofisi za wakala wa kusafiriashia kitu ambacho kwa sasa haiwezekeni kutokana na eneo la kituo kipya kutokuwa na majengo.

Hali ni tofauti kwani wakati wasafiri na wasafirishaji wakilalamika madereva wa boda boda wao wanaona kuwa hiyo ni fursa kwao kwani wanapata kpato kikubwa kwa kuwasafirisha abiria hadi kituo hicho kipya au kwenye kituo cha pili ambacho kipo Stesheni zakizungumnzia hilo mwakilishi wa waendesha bodaboda Abdalah Ngitu alisema kuwa kwa sasa kwao ni biashara mzuri kwani kutokana na umbali ba hali ya usalama wananlazimika kusafirisha abiria mmoja kwa kati ya shilingi 3000 hadi 5000 kwa muda wa usiku.

Akizungumzia malalamiko hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Nachingwea,Arbogast Kiwale alikiri na kudai kuwa kwa sasa halmashauri imeamua kufungua kituo hicho na kuwa tayari ujenzi wa mahali pa kupumzikia abiria lipo kwenye hatua za mwisho na kutarajiwa kuwa limekamilika muda mfupi ujao.
Sehemu ya Mabasi yakiwa yamepaki kwenye kituo hicho.
Abiria
Vibao vinavyoonyesha namna ya mabasi yatakavyoegeshwa,japo hakuna hata moja lililopo.
Basi zikipishana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2013

    haya ni masihara; mbona kuna nyasi tu? uongozi wa halmashauri woote yabidi ujiuzulu; wameshindwa kuwajibika. Yani unawapeleka Watanzanoa sehemu ambayo haina huduma??? Unategemea nini? Ivi siye Watanzania tunafanywa kama wanyama? Wanyama tu wanastahiki haki yao. Mambo mengine hatuhitaji semina toka USAID n.k. Mbona tunaleta mchezo??? Inasikitisha sana. Wananchi wakiandama mutasema munaleta fujo wakati wanateseka...

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2013

    Miji yote Tanzania inakabiliwa na ongezeko la watu na msongamano wa magari. Kuna moja sijalielewa ambalo mimi nilidhani lingesaidia kupunguza msongamano wa magari binafsi mijini, miji mingi inahamisha vituo vya magari ya abiria kutoka katikati ya miji kuvipeleka pembezoni! Hata kama wanaopanga hivyo wanauwezo wa kumiliki magari haiwasaidii kwa sababu watu watavutiwa zaidi kundesha magari yao katikati ya miji na hivyo kuongeza msongamano. Nilidhani kwamba kuviimarisha ikiwa ni hata kununua maeneo yanayovizunguka ili viendane na mabadiliko yanayotea ingekuwa bora. Ama magari ya abiria kuegesha katikati ya miji ni hatari kama ilivyo kwa ndege? Nimeona Tanga, na ninaambiwa kituo cha Ubungo nacho kitahama kuelekea pembezoni au ndio kutokuwajali wale wenye uwezo mdogo? Au ndio kupunguza kuongezeka kwa watu wa hali chini mijini. Kumbukeni hao ndio wanakufanyieni kazi ambazo mnaziona si za hadhi yenu, hivyo kuwaongezea ugumu wa maisha maana yake mtalazimika pia kuwaboreshea maslahi yao ili waweze kubaki mijiini kwa njia zilizohalali vinginevyo ni matatizo.

    sesophy

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2013

    Jamani si wangemwaga angalao changarawe na kujenga vibanda vya kupumzikia abiria wakatia wakisubiri usafiri. Hapo mvua ikinyesha ilo tope sidhani kama kuna basi litaondoka na abiria pamoja na mizigo yao wataloana.
    Bongo kila kitu kinafanywa holela tu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 12, 2013

    MBONA SIIONI HATA VYOO HAPO KITUONI!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 13, 2013

    Ohoooo!

    Je,

    -mtu skihikwa na haja atajisaidia wapi hapo?,
    -njaa ikiuma atakula wapi?,
    -mtu anaumwa ghafla akiwa safarini atapata huduma za dharura vipi?

    Halmashauri na Serikali za Mitaa mlitakiuwa muwekeze kwanza kwa vitu muhimu kama Migahawa, Vyoo, Maduka, Huduma za Dharura kama Zahanati na ikiwezekana sehemu za Mapumziko au nyumba za Wageni kabla hamjawatoa watu Stendi kamili na kuwagwaga Uwanjani!

    Hiyo ni Stendi au Uwanja wa Mazoezi au Ligi za Mchangani?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 13, 2013

    Hii ni ile tabia ya kiupenda kufiklia malengo kwa nji za mkato.

    Huku Stendi ikiwa ni Uwanja wa manyasi tu, hapo utasikia Korosho zimesha kusanywa zimeshauzwa huku Wakulima wakipewa vikaratasi na wakiwa hawaja kamilishiwa fedha zao!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 13, 2013

    Angalieni madudu ya Uongozi:

    Mnawatoa watu Mijini kwenye huduma za muhimu mnahamishia Stendi ya Mabasi hukooo majanini ambako hata Choo cha kujisadia mtu akibanwa hakuna!

    Hivi Uongozi Nachingwea mnazo akili timamu?

    Ile mtu akimeza bakuli moja la maharage, kikombe cha chai na andazi moja muda si mrefu wakati hata basi halijafika Kituoni anaweza kujisikia kujisaidia!,,,sasa ikitokea hali hiyo mtawasaidia vipi abiria huko Kituo kiya?

    Je, abiria wakati anasubiri basi halijafika akijisikia kuharisha ghafla mtamsaidia vipi hapo ni majanini na Uwanjani wakati hakuna hata Kichaka cha kujibanza na kujisaidia?

    Muelewe ya kuwa watu wanasafiri wengine wakiwa wagonjwa ama unaweza kutoka kwako ukiwa mzima ukifika Stendi ya Basi usijisikie vizuri na ukahitaji hata Kidonge kimoja umeze ,je Maduka ya dawa yapo hapo?

    Mngeweka angalau Huduma muhimu kwanza hapo ndio mhamishie Stendi ya Mabasi mfano

    1.Maduka ya Vocha za simu na Dawa,
    2.Migahawa ya vyakula,
    3.Mabanda ya kupumzikia abiria
    4.Vyoo na mabafu,
    5.Zahanati,
    6.Tawi la Ofisi yenu ili mfikiwe,
    7.Kituo cha Polisi na Usalama.

    Je Ushuru mliokusanya hapo nyuma fedha hizo mnafanyia nini?

    Je hivi kweli mnawatendea haki Wananchi?

    Kwa nini Mnagombea Uongozi wakati uwezo wa Utawala,kufikiri na Ubunifu wa kutumia Madaraka hamna?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...