Mahmoud Ahmad Arusha.
Jeshi la polisi mkoani hapa limefanikiwa kukamata magunia 30 ya bangi huku askari wawili wa jeshi hilo mkoani hapa wakikamatwa wakati wakisindikiza magunia 18 ya madawa ya kulevya aina ya mirungi kwenye mpaka wa nchi na Kenya Holili mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa jeshi hilo mkoani hapa kamishna wa msaidizi wa polisi Liberatus Sabas alisema kuwa mnamo tarehe 19 mwezi huu huko mpakani mwa nchi ya Kenya na Tanzania Holili mkoani Kilimanjaro askari wawili wa Jeshi hilo mkoani hapa Koplo Edward na Mwenzake pc.George walikimatwa akisindikiza mirungi magunia kumi nane.
Kamanda Sabas alisema kuwa watuhumiwa hao wapo mkoani Kilimanjaro na taarifa zao anazo kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz alibainisha kuwa jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na bangi magunia 30 katika msako mkali walioufanya kwenye kata ya Ngarenanyuki wilayani Meru.
Sabas alibainisha kuwa wengine wawili walikimbia na jeshi hilo linawatafuta katika hatua nyingine jeshi hilo limakamata gari lenye namba za usajili KBQ372V lililoibiwa nchi jirani ya Kenya majira ya saa 6:30 usiku huko wilayani Longido.
Kamanda Sabas alisema kuwa katika kupambana na mitandao ya madawa ya kulevya walifanikiwa kuwakamata askari hao na kuwataka watanzania na wakazi wa mkoa huu kutoa taarifa zitazosaidia kumaliza matukio ya kiuhalifu mkoani Arusha kwani Arusha bila ya madawa ya kulevya inawezekana na nchi vile vile pia
Kwa kweli khali ya jeshi la Polisi inazidi kuwa mbaya hapa nchini. Wao ndio wanakuwa wasimamizi wakuu wa maovu badala ya kuwa walinzi. Afande Kova tunaomba uvalie njuga swala hilo. Hapa Kawe kituo cha Police ndio hapafai kabisa. Ukireport tu tukio unatakiwa kutoa 50,000 ati ya kusaidia kuandika statement. Ukimfikisha mtuhumiwa kituoni, wewe uliyempeleka mtuhumiwa utaombwa fedha na mtuhumiwa mwanyewe pia ataombwa fedha mara 2 ya ile uliyoombwa wewe na kuelekezwa nini afanye ili atolewe. Nilibiwa nyumbani nikaenda kureport Kawe na mshukiwa nikamtaja. Wakaniomba laki 2 ili wakapekuwe nyumbani kwake na nikawawekea na mafuta. Bahati vitu vingi vilivyoibiwa nyumbani vilikutwa kwa mtuhumiwa,isipokuwa fedha basi niliambiwa nichukue vitu vyangu na niende nyumbani. Nikashangaa sana nilidhani vitu hivyo vitatumika kama ushahidi mara mshutumiwa atakapopelekwa mahakamani. Wakanieleza niende siku ya Jumatatu, maana siku hiyo ilikuwa ni Alhamisi. Siku ya Jumapili mtuhumiwa akapita nyumbani akiwa na wenzake, niliogopa sana. Akasema ametoka kwa laki 6, alipita tu kunijulisha kuwa yuko nje. Sikuona haja ya kwenda Polisi hiyo Jumatatu. Kwakweli ndio maana sasa hivi watu huamua kuchukua sheria mkononi. Jamani kama hatua za haraka hazitachukuliwa basi kwa kweli khali inatisha. Afande Kova na serikali, wizara ya mambo ya ndani angalieni jeshi la Polisi kwa jicho la tahadhari.
ReplyDeletehii ndio bongo bwana.chezea bongo wewe
ReplyDeletekWA MANTIKI HII SWALI NI JE MHALIFU ATAMKAMATA JE MHALIFU MWENZAKE?
ReplyDeleteTuunde POLICI WA POLICI
ReplyDeleteTunaelekea Patamu sana jamani sasa N'nji hii naapa! NGoma Inogile!
ReplyDeleteTz huko hakuna polisi. wote njaa tupu.
ReplyDeleteUkisikia uhalifu wowote lazima polisi yuko nyuma kama mlinzi wa uhalifu. Hapa TZ ukisikia uhalifu umetokea mahali wala huna haja ya kuumuza kichwa. Ukivamiwa ukibiwa ujue polisi wanajua.Hivyo hata ukienda kutoa riport hakuna msaada utakaopata zaidi ya kukukamata wewe kama mhalifu kwa sbb umetoa riport.