MSHAMBULIAJI Mrisho Ngasa amemwaga wino wa kuichezea klabu ya Yanga kwa dola 30,000 ikiwa ni mkataba wa miaka miwili.
Habari zilizotufikia chumba cha habari cha Globu ya Jamii leo hii zimesema kuwa tayari uongozi wa Yanga umeshampa kitita cha dola 10,000 mshambuliaji huyo ambaye aliondoka kwa mbwembwe kwenda Azam kwa dau la milioni 50,000.
Chanzo hicho kimedai kuwa Ngasa bado anaidai klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani kitita cha dola 20,000 ambacho aliahidiwa kukabidhiwa mara atakapotua rasmi ndani ya klabu hiyo.
Uongozi wa Yanga leo umemtambulisha rasmi Mrisho Ngasa kwa kurejea kundini baada ya kumaliza mkataba wake na Azam ambao walimpeleka kwa mkopo Simba ambako ametukimikia klabu hiyo ya wekundu wa Msimbazi kwa muda wa mwaka mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari Ngasa ambaye amekabidhiwa jezi iliyokuwa na jina lake na Katibu mkuu wa klabu hiyo Laurance Mwalusako alisema "Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kurudi tena Yanga, klabu ambayo nina mapenzi nayo toka utoto, nawashukuru viongozi wa Yanga waliofight hasa rais Kifukwe (Francis) kuhakikisha wananirudisha kundini.
"Nilipokuwa Azam, Simba nilicheza kwa uaminifu mkubwa lakini viongozi hawakuwa na imani na mimi kwa vile nina mapenzi na Yanga, ni kweli naipenda Yanga lakini hata siku moja sikucheza unazi, nilicheza kwa uaminifu kwa vile mpira ni ajira yangu, mapenzi yanafuata lakini viongozi hawakuliona hilo.
Kuhusu kusaini mkataba na Simba ambapo alipewa dola 25,000 pamoja na gari aina ya Verosa Ngasa alisema "Sina mkataba na Simba na sijawahi kusaini mkataba na Simba, mkataba wangu ni Azam na Azam walinipeleka Simba kwa mkopo.
Akifafanua jambo hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga Abdallah Bin kreb alisema "Shilingi 25 milioni zilizotolewa na Simba ilikuwa ni ada ya kumtoa Azam kwenda Simba na gari alilopewa ilikuwa ni ushawishi tu ili akubali kucheza Simba klabu ambayo hakuwa na mapenzi nayo."
Alisema kama Yanga hawana kinyongo na mchezaji huyo ambaye aliitosa timu yao na kwenda kusaka maslahi Azam na kwa wapinzani wao na kwamba hata penati aliyoisababisha katika mechi dhidi ya wapinzani wao iliyochezwa Jumamosi na Yanga kuibuka na mabao 2-0 imedhihirisha uamifu wa Ngasa katika timu alizochezea.
Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zakaria Hanspop
alisema "Mkataba wetu na Ngasa upo wazi tena unasema wazi utaanza pale ambapo mkataba wake na Azam utakapomalizika, hatujaingia mkataba juu ya mkataba kama Yanga wanavyodhani.
"Yanga wamezoea fujo wanafanya mambo kama vile TFF ni mali yao wanajua watabebwa, kwanza wao ndio waliomwambia Ngasa sio mali kitu, ameshuka thamani wakati ule sisi tulitaka kutoa milioni 20 wao wakambiwa waongeze tano iwe 25,000 milioni ili wamchukue walikataa na kusema hana thamani ya hela hiyo imekuwaje sasa? alisema kwa kuhoji na kuongeza "Kuna watu wanampotosha Ngasa na tulishamwambia kabisa mchezaji mzuri lakini atajikuta anishia pabaya, sisi tutafuata sheria TFF ndio watakaoamua.
Ndio maana Ngasa hakucheza kwa bidii siku ile alijua anachokifanya. Hawezi uifunga timu yake. Haya hilo ndio soka la bongo
ReplyDeleteMie naona mpira wake ndo umekwenda KABURUNI.
ReplyDeleteTANZANIA WACHEZAJI WENYE AKILI NI WAWILI TU TUNAOJIVUNIA NAO.SAMATTA NA ULIMWENGU (MUNGU AWASAIDIE WAFIKE MBALI ZAIDI YA HAPO)SIO HAWA MAKANJANJA WENYE USHAMBA WA KUTANGULIZA MAPENZI YA TIMU BADALA YA FUTURE...AZAM WAMEKUFANYA NGASA UKAKABWA NA RIO FERDINAD WA MAN U.UKACHEZA SAMBAMBA NA ROONEY PALE WALIPOKUPELEKA MAREKANI KTK CLABU RAFIKI WA AZAM KWA MAJARIBIO YA SOKA LA KULIPWA HUKUSTAHILI KUBUSU JEZI YA YANGA HADHARANI WAKATI UNAJUA WALIKUA NA NIA NJEMA YA KUKUEXPOSE KTK SOKA LA DUNIA.FURSA ILIYOJE HIYO.NA NATUMAI ANGEKUA SAMATTA KTK FURSA HIYO SASA TUNGEKUA TUNAMUANGALIA KTK SUPER SPORT 3 LAKINI KWA KUA UNA MAPENZI YA KISHAMBA NA YANGA BADALA YA SOKA AKILI YAKO IMEFUNGWA HAPA HAPA BONGO...ACHA USHAMBA WEWE SIKU HIZI SOKA NI PESA SIO MAPENZI NA TIMU.
ReplyDeleteMpira Pesa baba. Tengeneza maisha Ngasa wajinga ndio waliwao
ReplyDeleteKwa bahati mbaya wachezaji wakitanzania hawakumbuki ule usemi wa "fainali uzeeni" kaka zao waliowatangulia walifanya makosa kama haya ya mapenzi wa timu na sasa wanahangaika mitaani!!!
ReplyDelete