Msajili wa bodi ya makandarasi nchini (CRB), Eng. Boniface Muhegi (kulia) akisisitiza jambo alipokua akitangaza kuhusu mkutano mkuu wa majadiliano wa bodi hiyo unaotarajiwa kuanza alhamis ya wiki hii jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni msajili msaidizi, Utafiti na Maendeleo, Eng. Magesa Bairi (katikati) and msajili msaidizi wa bodi hiyo, Utawala na Fedha, Bw. Rhoben Nkori.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini (CRB) imewataka makandarasi hapa nchini kuhudhuria kwa wingi kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa majadiliano wa bodi hiyo unaotarajiwa kuanza alhamisi wiki hii jijini Dar es salaam.

Msajili wa Bodi hiyo injinia Boniface Muhegi ametoa wito huo mjini Dar es salaam jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano huo ambao kwa mwaka huu utaangalia kwa undani mafanikio na changamoto katika sekta ya ujenzi Tanzania miaka kumi na tano tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo.

Amesema washiriki wa kada mbali mbali kutoka sekta ya ujenzi wanakaribishwa kwenye mkutano huo kwani mkutano huo utakuwa na manufaa makubwa kwao ikiwamo kusaidia kuwapandisha madaraja na kupata alama katika maendeleo ya fani yao.

Ameongeza kuwa washiriki kutoka nchi za Kenya,Uganda,na Rwanda wamealikwa ili kuweza kubadilishana uzoefu na washiriki wa ndani. “Tunahamasisha ushiriki wa wakandarasi toka sekta binafsi na umma,” alisemana kuongeza kuwa pia patakua na maonyesho ya huduma na vifaa mbalimbali vya sekta hiyo.

Amedokeza kuwa sekta ya ujenzi Tanzania imepiga hatua kubwa toka kuanzishwa kwa bodi hiyo miaka 15 iliyopita kwani kulikuwa na makandarasi wapatao 1000 kulinganisha na sasa ambapo kuna jumla ya makandarasi 7000.

Ametaja mafanikio mengine kuwa ni kuongezeka kwa ubora na uwingi wa kazi za ukandarasi wa ujenzi akitolea mfano ongezeko la minara ya mawasiliano ya simu za mkononi ambayo imetapakaa karibu nchi nzima, barabara na majengo ya kisasa. “Pamoja na vikwazo mbalimbali, tumepiga hatua kubwa,” alisema.

Pamoja na maendeleo hayo pia ametaja baadhi ya changamoto ambazo zitajadiliwa kwenye mkutano huo ikiwemo kujenga uwezo wa wakandarasi wazalendo, kutofuata kanuni na sheria mbalimbali.

Mada nne zitawasilishwa kutoka kwa wadau mbalimbali zote zikilenga changamoto na mafanikio katika sekta ya ujenzi Tanzania ndani ya miaka kumi na tano.

Mapendekezo ya mkutano huo yatapelekwa kwa wadau husika na baadae kufuatilia utekelezaji wake.

Pia mkutano huo utapitia utekelezaji wa maazimio ya mkutano uliopita ikiwepo la madeni ya makandarasi.

Takwimu zinaonyesha kwamba sekta ya ujenzi inachangia asilimia saba ya pato la taifa huku ukuaji wake kwa mwaka ikikadiliwa kuwa ni asilimia kumi na moja ikiwa ni sekta ya pili kwa kasi ya ukuaji huku sekta ya madini ikiongoza.

Asilimia sitini ya bajeti ya maendeleo nchini inakwenda kwenye sekta ya ujenzi huku asilimia themanini ya fedha hizo zikienda kwa wanachama wa bodi ya usajili wa mandarasi wa ujenzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...