Balozi wa Tanzania BENELUX na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye rangi ya taifa) akiendesha Mkutano wa Wadau wa Ushikirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership) wa Brussels. Kushoto kwa Balozi Kamala ni mhe. Alhaji Muhammad Mumuni Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pacific. Kulia ni Dr Smith Mihela Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Ushirkiano kwa Manufaa ya Wote. Mkutano umefanyika leo Brussels.
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Mabalozi wa Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote - Brussels Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai) akimkabidhi Ilani ya Ushirkiano kwa Manufaa ya Wote Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kibiashara Cha Jumuiya ya ulaya Bibi Sandra Gallina. Kulia kwa Bi. Sandra ni Dr. Mihela Smith Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership). Mabalozi wa nchi za Afrika, Karibiani na Pacific na wadau wengine wamekutana leo Brussels, Ubelgiji kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa Ushikirikiano kwa Manufaa ya Wote utakaofanyika Dar es Salaa mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...