MTANZANIA mwenzetu marehemu Shaaban Robert anaandika;
” Wasadikika wana desturi ya kutafuta fimbo baada ya kuumwa na nyoka. Tumekwisha umwa na nyoka kwa matendo yetu mabaya ya zamani.

Nyoka mwenyewe amekwishakimbia. Hapatikani kwa kujilipiza kisasi, lakini, sumu yake imebakia katika jeraha tulilolipata. Sasa, shauri lililo jema ni kuzuia sumu hii isienee miilini mwetu ikaleta kifo.
Maovu yana hatari kubwa kukaa kati yetu. Tumedumu nayo kwa muda mrefu. Hayakutuletea faida ila hasara, huzuni na kilio siku zote.”- Shaaban Bin Robert.


 Ndugu zangu,
Yanayotokea Mtwara yanatuletea mashaka kama taifa.  Linalohitajika sasa si tamko la Serikali tu, bali, tamko letu Watanzania kwenye mioyo yetu, kwamba, pamoja na haki yetu ya kimsingi ya kudai  haki, lakini, lililo la hekima na busara ni kutumia njia mujarab za kuitafuta haki hiyo. 

Na njia hiyo haiwezi kuwa ni matumizi ya nguvu ikiwamo kufanya vurugu. Hivyo, kufanya maovu ikiwamo kutoa roho za wenzetu na uharibifu wa mali, iwe imefanywa na wananchi au Serikali.

 Kama Watanzania huu ni wakati wa kufikiri kama taifa. Hii ni Nchi Yetu. Huu si wakati wa kufikiri kwa mitazamo ya kiitikadi au kiimani. 

Yanayotokea Mtwara yana madhara kwa nchi nzima, na yakiachwa bila kupatiwa ufumbuzi  wa haraka, yatatawanya sumu mahala pengine pia.
 Ni wakati wa Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Chama Tawala, Viongozi wa Vyama Vya Upinzani , Viongozi wa kidini na kwa kuwashirikisha wazee wa Mtwara, kutoa matamko yatakayosisitiza umuhimu wa kutumia majadiliano  katika kupata ufumbuzi wa tatizo lililopo.

 Tukumbuke, kuwa nchi yetu ina mipaka, hivyo basi, ina maadui pia. Tusipotanguliza hekima na busara, yumkini tunaweza kutoa nafasi kwa maadui kutugombanisha zaidi. Na hivyo  ikawa hasara zaidi kwetu , na faida kwa wengine.

 Hakika,tunaweza kuyamaliza yetu kwa mazungumzo. Tuianze kazi hiyo sasa.

 Maggid Mjengwa,
Iringa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2013

    Huyu majid kila ninapojaribu kumuelewa hasomeki, na simuelewi kwakweli kwa kila mada anayoitoa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2013

    Ndugu Michuzi, Nakubaliana na hayo yote aliyoyasema Mjengwa. Kama mtanzania naomba kushauri yafuatayo:
    1.0 Viongozi wa serikali wawaelimishe vizuri wananchi wa Mtwara, inaonekana hakuna mawasiliano mazuri kati ya serikali na wananchi. Waziri wa Nishati alipaswa kuelezea issue nzima ya matatizo yaliyotokea na jinsi yalivyotatuliwa na jinsi yatakavyowasaidia wananchi wa Mtwara na Tanzania nzima. Kilichofanyika ni kuwa waziri alikuwa anaelewa kabisa kitakachotokea lakini akaamua kuwa bold. Hapana hawa wananchi wanapaswa waelezwe kila hatua, ni haki yao pia.
    2.0 Kuwe na mawasiliano ya karibu kati ya waziri na wananchi-sasa hivi hakuna mawasiliano ni kwamba waziri anajaribu kuonyesha ubabe na watu wa huko Mtwara wana hasira naye sana (Si yule yule waziri aliyewaita wana-Mtwara "WAPUUZI".
    Rais anafanya kazi nzuri na ni msikivu lakini hao wanaomsaidia wana mentality ya kizamani kwamba 'tutawadhibiti hawa', ndugu zangu haya mambo ya huko Delta state Nigeria, Colombia, philipines,IRA n.k yalianza hivi hivi,kidogo kidogo watu wakawa wanauawa baadaye wanajenga hasira....Ninyi viongozi wa serikali mnafikiri msipowashirikisha wananchi wa Mtwara mtafika mbali? Tuwashirikishe wananchi tukiwashirikisha hatutaona sabotage ya miundo mbinu ya gesi na wananchi watafurahi na kuilinda ipasavyo, vinginevyo hata tukiweka jeshi gani, miundo mbinu itaharibiwa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2013

    Mdau wa kwanza... jaribu kwenda hospitali hizo ni dalili za kudata/uchizi... seriously kwa sababu Mjengwa amesomeka vizuri, mdau wa pili umezungumza ukweli mtupu.. watu kama wewe ndo tunahitaji hamlaumu bali mnatoa suluhisho au mawazo mazuri

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2013

    anan wa mwanzo, Majid haeleweki au wewe huelewi? Ana MS huyo. Wewe ulipata div ipi shuleni au hata seko hukwenda?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2013

    Fujo siyo suluhisho, imefika kipindi vyama vya upinzani, pale tunapotaka kudumusha amani, umoja na utulivu muwe pamoja na serikali iliyopo madarakani, maana imechaguliwa kidemokrasia. Yakitokea maafa, nyinyi pia hamtapona maana laana zipo ni kama Nyerere alivyosema ukipanda mbegu ya chuki ya watu wapenda fujo, kumbuka na wewe ukichukua dola uwe tayari kukubali uchochezi huo toka kwa chama kinachotawala sasa na sio kuanza jazba ya kuwaweka kizuizini. Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, kwa hili kuweni upande wa serikali kama walivyo wapinzani wa NCHI ZILIZOENDELEA...

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 23, 2013

    Kwa hili la Mtwara safari hii sio la kuunga mkono. Kweli hawajatenda jambo zuri, ni la kulaani,kama ujumbe ulishafika siku nyingi. Kuna kuwa na subira katika maisha. Lakini pia lazima waelewe gas ni ajili ya watanzania wote kama zilivyo rasilimali nyingine. Zinatumika kwa mipango ya kitaifa sio wanamtwara tu. hacheni huo ubinafsi. kama ni wanasiasa wanawadanganya tu. undeni kamati za ufatiliaji zikishindwa mtapata jibu la kufanya njia mbadala. lakini ndugu zetu mnakaa kwenye redio kusikiliza nini alafu maamuzi ni kufanya fujo. fujo hazisaidii tunaishia kuuana na kuharibu mali na kikubwa kuweka nafundo ya chuki rohoni. na nyinyi wapinzani hiyo sio njia nzuri ya kutaka kadaraka, hivyo mnakuwa mmeishiwa na hoja. Itafika wakati mtachokwa na wananchi.
    KUMBUKA BOB MARLEY: YOU CAN FOOL SOME PEOPLE SOMTIMES BUT YOU CAN NOT FOOL ALL THE ALL THE TIME.
    TANZANIA NI YA WOTE NA RASILIMALI NI ZA WOTE

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 23, 2013

    Serikali inatumia mabavu na haitaki kusikiliza wananchi. Kuna ubaya gani wa gesi kusafishwa kwanza Mtwara na baadae kupelekwa huko inapopeekwa? Kinachotaka kufanywa sasa ni kama vile korosho zao zinapopelekwa India kuwa processed huko. Kuwaambia sasa kuwa watajengewa kiwanda cha sementi na ahadi kem kem ni kuwadhalilisha, ni kama kumdanganya mtoto na pipi! Kwa nini hivyo viwanda havikujengwa hapo awali ila sasa ndipo wanaahidiwa? Ni kwa sababu ya kutaka kusafirisha gesi ndio wanaahidiwa watajengewa hivyo viwanda! Kusema kuwa wana Mtwara hawataki gesi isitumiwe na Watanzania wengine ni kupotosha ukweli. Wao wanataka gesi ianze kuwa processed pale, na si kujenga bomba ikawe processedkwengine! Wanaokazania kujenga bomba la kusafirisha mafuta wana lao jambo!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 23, 2013

    wanasiasa wetu hawaelewi kuwa unapopanda mchicha unavuna mchicha so hizo chuki wanazopandikiza kwa wanachi hata wao wakiingia madarakani zitawasumbua.nadhani kuwa na rasimlimali nyingi si kigezo chakuendelea coz kama hivi ndivyo basi mwanga wasingekuwa na maendeleo na shy ndio wangekkuwa na maendeleo.maendeleo ya eneo husika yanletwa na kuanzia diwani hadi uongozi wa juu.sasa kama watu wanashindwa kusimamia kidogo wanachopata wanategemea hiyo gesi ndio itafanya miujiza?na kusema wa mtwara wasikilizwe ni kumaanisha kuwa mikoa yote yenye rasilimali basi zisitoke zibaki hapo coz hata wengine wakisikia wamesikilizwa na wao watadai.na nyie wanachi wa mtwara wenzenu wana wachochea wako mbali na wameisha jianda kwa safari nyie mnapo pa kwenda kwanini ukubali kizazi chako kiangamie kwa watu wnaotaka kutimiza matakwa yao ya kisiasa.

    ReplyDelete
  9. cha msingi wajaribu kutoa elimu ya kutosha kwa watu wa mtwara ni kwa vp wata nufaika na hyo gesi yao adhani bado hawajatambua gesi hyo itawafaidisha vp unajua hakuna ki2 kinacho umiza kama una mgodi halafu wengine wanachimba bila mwenye mgod kujua faida atakayo ipata waziri ni kama ametumia force alitakiwa kueleza kwa kina jinsi watu wa mtwra watakavyo nufaika na jinsi nchi itakavyo faidika likifanyika hili sidhani kama vurugu zitaendelea. Vurugu hazifai jaman

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...