WATANZANIA WOTE MNAOMBWA MJITOKEZE KWA WINGI KATIKA KUSHANGILIA TIMU ZETU . MASHINDANO YANAANZA JUMAMOSI HII TAREHE 01/06/2013 kwenye MEMORIAL PARK GROUNDS, EAST LONDON.
 TUNAWATAKIA KILA LA KHERI TIMU ZOTE KOMBE LIRUDI UBALOZINI KUTOKA KATIKA TIMU MOJAWAPO YA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA. 
 KWA HABARI ZAIDI TEMBELEA : 
www.africannationscupuk.com

  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Peter Kallaghe akikabidhiwa Kombe na Waandalizi ikiwa kama ishara ya Timu za Zanzibar Islands na Tanzania kushiriki katika mashindano hayo. Pichani wa kwanza kushoto ni  Kocha / Kiongozi wa Timu ya Tanzania Abdul Kassim akifuatiwa na kijana Dula Kapteni wa Tanzania Team. Kushoto ni Mkurugenzi wa  Tanzania Trade Centre Bw. Yusuph Kashangwa.
 Ballozi Kallaghe akikabidhiwa Kombe na Waandalizi ikiwa kama ishara ya Timu za Zanzibar Islands na Tanzania kushiriki katika mashindano hayo. Pichani wa kwanza kushoto ni  Kocha / Kiongozi wa Timu ya Tanzania Abdul Kassim akifuatiwa na kijana Dula , Kapteni wa Tanzania Team. Pembeni ya Balozi ni Director wa Tanzania Trade Centre Mr Yusuph Kashangwa.
 Balozi Kallaghe akiwa katika picha ya pamoja na Waandaaji wa Shindano hilo litakaloundanisha timu za Nchi 20 za jamii ya Africa wanaoishi Uingereza. Pichani vilevile ni baadhi ya Viongozi wa Timu zetu za Tanzania na Zanzibar islands.
Balozi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Timu zetu na baadhi ya Vijana wachezaji, baada ya kuwakabidhi Kombe na Bendera ya Tanzania itakayopepea kwenye mashindano hayo kuanzia tarehe 01/06/2013 katika viwanja vya Memorial Grounds , Forest gate  na Fainali kuwa tarehe 15/06/2013 katika Uwanja wa Westham Football Grounds (Upton Park )

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2013

    Timu za Tanzania na Zanzibar islands.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2013

    Ivi mbona sielewi hapa yaani Timu ya zanzibar island na Tanzania?Ni kosa la ki-uandishi au ndio kukwepa kuitwa mchochezi?Haya bwana time will tell.

    ReplyDelete
  3. Mie nadhani itakuwa imekusudiwa Timu ya TANZANIA ni kutoka upande wa "TANZANIA BARA" na timu za "ZANZIBAR ISLANDS" ni mjumuisho wa timu za visiwa vyote vya ZANZIBAR kikiwemo kisiwa cha UNGUJA, PEMBA, TUMBATU, n.k. ndio hiyo TZ & ZNZ ISLES.
    By the way, kila la kheri kwa pande zote mbili,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...