Imeelezwa kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazofaidika na fedha kutoka benki ya Maendeleo Afrika (AFDB), hii ni kutokana na matokeo ya utendaji kazi wa kuridhisha katika matumizi ya fedha za miradi.
Hayo yamesemwa na mwakilishi wa benki ya AfDB nchini Bi,Tonia Kandiero wakati alipokutana na uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, ukiongozwa na Waziri, Profesa Sospeter Muhongo kwa lengo la kuzungumzia ushiriki wa benki hiyo katika uendelezaji wa sekta ya nishati nchini.
Kutokana na umuhimu wa Nishati kwa ajili ya kuinua uchumi wa nchi, Benki ya AfDB katika awamu nyingine ya fedha inayoanza mwaka 2014 inatarajia kutenga Dola za Marekani milioni 600 au zaidi kwa ajili ya kuendeleza sekta mbalimbali nchini ambapo nusu ya fedha hizo itatengwa kwa ajili ya kuendeleza sekta ya Nishati.
Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini,
Bw.Eliakim Maswi wakiwa kwenye mazungumzo
na Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo Afrika nchini, Bi.Tonia Kandiero
ambaye aliongoza ujumbe wa wataalam kutoka Benki hiyo kwa ajili ya mazungumzo
kuhusu upatikanaji wa fedha za kuendeleza sekta ya Nishati nchini.
Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini,
Bw.Eliakim Maswi wakiwa pamoja na wataalam
wa Wizara ya Nishati na Madini na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) wakijadili
kuhusu ushiriki wa Benki ya hiyo katika uendelezaji wa sekta ya Nishati nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...